Kenya kupiga marufuku mahusiano ya kimapenzi miongoni mwa maafisa wa polisi | ZamotoHabari.




Hatua hii ina nia ya kupunguza viwango vya uhalifu unaotokana na masuala ya mapenzi miongoni mwa maafisa hao, Waziri wa usalama wa Ndani alieleza hayo kwenye sherehe katika chuo kimoja cha polisi nchini humo.



Kanuni hizo kwanza zinahitaji kupewa idhini na Baraza la Usalama la Taifa, linalosimamia vikosi vyote vya usalama vya nchi hiyo, Fred Matiang’i alisema.

Ndani ya huduma ya polisi , mahusiano yalishapigwa marufuku miongoni mwa maafisa wa vyeo tofauti, alieleza.

Miezi michache iliyopita, kulikuwa na ongezeko la mauaji ya wapenzi, waziri huyo alieleza.

”Hatuwezi kufungia macho suala hili na kutokuzungumzia baadhi ya changamoto tulizonazo kwenye sekta ya usalama,” Bw. Matiang’i alisema.

Ofisi ya jinsia pia itatazama kesi za udhalilishaji wa kingono ulioripotiwa na maafisa polisi.

”Hapo baadaye, itakuwa ni kosa kisheria kwa polisi kuwa na mahusiano au kuoana na afisa polisi mwenzie. Ikiwa itatokea maafisa hao wawili wakapendana, basi mmoja wao atapaswa kuacha kazi,” Gazeti la Star lilimnukuu waziri huyo akisema.

Walakini, Wakenya wanauliza ikiwa sheria zinaweza kuwazuia watu wazima wawili wasipendane. Wengi waliamua kutumia mitandao ya kijamii kutoa maoni yao kuhusu kauli ya waziri huyo .

Matiang’i alikuwa amesema, “Tutachukua mfumo sawa na ule wa jeshi la Kenya ambao unawazuia wanajeshi kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na wenzao.”

Matamshi ya Matiang’i yanakuja karibu wiki tatu baada ya mlinzi aliyekuwa akihudumu ofisini mwake kumua mkewe ambaye alikuwa afosa wa trafiki na kisha kujiua

Afisa huyo wa kikosi cha GSU Hudson Wakise alimuua mkewe kwa kumpiga risasi kabla ya kujiua kwa kujifyatulia risasi .

Mkewe baadaye alipewa taadhima za maziko ya polisi lakini Wakise alizikwa bila polisi kuwepo .

Katika hotuba yake ya tisa juu ya janga la Covid-19, Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta alielezea wasiwasi wake juu ya “kuongezeka kwa mivutano ndani ya nyumba (zetu).”

Rais aliamuru Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Uhalifu kuchunguza visa vinavyozidi vya unyanyasaji wa kijinsia na ukiukaji wa haki za watoto


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini