Wakati leo kikosi cha Simba kikiwa na kazi ya kusaka mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar, kikosi hicho kinatarajiwa kuwakosa nyota watano ambao ni Francis Kahata pamoja na Ibrahim Ame.
Kahata yeye amesajiliwa na Simba kwa ajili ya mechi za kimataifa ambapo Simba imetinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imepangiwa na Kaizer Chiefs.
Ame atakosekana leo kwa kuwa amefungiwa na Kamati ya Masaa 72 kwa kosa la kumzuia mwamuzi wa pembeni katika mchezo wa ligi dhidi ya Gwambina.
Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Gwambina Complex na ubao ulisoma Gwambina 0-1 Simba.
Wengine ni pamoja na Gadiel Michael, Ally Salim na David Kameta, 'Duchu' hawa hawajawa fiti kwa kuwa wamekosa mechi kwa muda mrefu.
Kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Meneja Patrick Rweyemamu amesema kuwa hakuna majeruhi ndani ya kikosi hicho na maandalizi yapo sawa.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments