
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akimsikiliza Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Khalifa Abdulrahman Almazrzouqi kbala ya kuagana mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaa ambapo wamezungumzia mikakati ya kukuza Utalii nchini ikiwemo kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo nchini katika ndege za Emirates na vyombo vya habari vya kimkakati vilivyopo Uarabuni ili kuteka soko la Utalii katika Umoja wa Falme hizo.

Waziri wa Maliasil na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Menejimenti ya NMB makao makuu katika kikao kilichofanyika leo mapema Jijini Dar es Salaam kilicholenga kuboresha mahusiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Benki hiyo ili kufanya kazi kwa pamoja katika kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa kuwawezesha kufanya malipo kupitia Benki hiyo.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA




0 Comments