AMINA SWEDY AJIKITA KUSAIDIA WALIMBWENDE TENA | ZamotoHabari.

Na Khadija Seif , Michuzi Tv
WALIMBWENDE watakiwa Kuonyesha jitihada za dhati katika kutetea Mataji yao ili kuweza kuwapa Moyo wadhamini kuendelea kujitosa kila Mwaka Kudhamini Mashindano hayo.

Akizungumza na Michuzi Tv Moja ya Wadhamini katika Mashindano ya ulimbwende Mkurugenzi wa kutengeneza Mapambo pamoja na Kadi (itsallaboutcards), Amina Swedy amesema kutoa udhamini kwa Mashindano hayo ina mjengea uwezo pamoja na kujifunza vitu vingi kupitia Wasichana wadogo wenye ndoto ya Kufika mbali.

"Msukumo wangu wa kukubali kutoa Ushirikiano Kwenye Mashindano ya Ulimbwende kwa sababu napenda kuona urembo ukipewa heshima na kuonekana kama ajira zingine hivyo najitahidi kutengeneza Mataji ambayo yana hadhi pamoja na nakshi nakshi zenye kuleta mvuto pindi Mrembo anapolivaa naona kweli Warembo wanastahili vitu vizuri hata hivyo wanaonyesha nidhamu Sana pamoja na kufurahia kile kitu ambacho Kama wadhamini huwa tunakitoa."

Pia amewatoa hofu Wazazi na walezi ambao wanaochukulia urembo Kama uhuni.

"Urembo sio uhuni ni heshima pia kwa Sasa kupitia Sekta ya Urembo imekua ikitoa ajira nyingi Sana na hata hivyo kupitia urembo tunazalisha viongozi ambao wanakua ni mfano mzuri wa kuigwa katika jamii yetu."

Aidha, amesema kuwa kwa Mwaka huu amedhamini kwa mara nyingine tena Shindano la Miss Higher Learning na anategemea kutoa ushirikiano wa dhati katika shindano hilo litakalofikia kilele chake mapema mwezi Agosti mwaka huu.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini