Sekta ya Mifugo kwenda kwa Kasi Tanzania Bara na Zanzibar | ZamotoHabari.

*Vibali vyote kutambulika kwa pande zote vile vinavyohusu Sekta ya Mifugo

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
WIZARA Mifugo na Uvuvi -Sekta ya Mifungo na Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji, Mali Asili,Mifugo Zanzibar zimekutana kufanya ushirikiano katika Sekta ya Mifugo kwa kukuza uchumi baina ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kukutana kwa Wizara hizo ni pamoja kutoa vikwazo ambavyo kimsingi vilikuwa havileti tija kwenye biashara wakati nchi ni moja.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi -Sekta ya Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa vibali vinavyotolewa kwa pande mbili lazima vitambulike kwa pande zote mbili.

Profesa Ole Gabriel amesema kuwa suala la udhibiti litazingatiwa ikiwa pamoja na kuimarisha watalaam kwa pande zote ili kuweza kutatua changamoto ambazo zimejitokeza.

Aidha amesema kuwa sekta ya Mifugo ina fursa nyingi na hivyo wawekezaji kwenda kuwekeza Zanzibar.

Profesa Ole Gabriel amesema Ng'ombe Milioni 3.9 huku Maziwa yakizalisha zaidi ya lita bilioni tatu ambapo wafanyabiashara na wawekezaji watumie fursa kwenye nyama na Maziwa na Mifugo mingine.

Amesema katika makubaliano waliojiwekea ni sita ambapo kwanza ni kujenga uwezo wa mabaara ya Mifugo,ZALIRI na TALILI kuimarisha katika utafiti na kutoa matokeo katika utekelezaji,Udhibiti wa Mazao ya Nyama na Maziwa,kubadilishana Walimu wa Vyuo vya Mifugo na maeneo mengine.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji Mali Asili, Mifugo Zanzibar Maryam Juma Sadalla amesema kuwa wanatajia kuongeza ajira 300 katika Sekta hiyo.

Katibu Mkuu Zanzibar Sadalla amesema kuwa serikali ya Mapinduzi imefunguka milango katika Sekta hizo kwenda kwa kasi katika kuinua wananchi kiuchumi na serikali kuongeza uwigo wa mapato

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa kwa sasa wamefungua milango ya ushirikiano kwenda kuchochea maendeleo ya uchumi.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini