BANDARI TANGA WATUMIA MAONESHO YA 8 YA BIASHARA KUELEZA HUDUMA WANAZOZITOA | ZamotoHabari.








KAIMU Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa maonyesho hayo


KAIMU Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire amesema watatumia maonyesho ya 8 ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga ili kuelezea huduma wanazozitoa kwa wananchi kwa sababu lango la bandari ni kurahisisha biashara.

Ngaire aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao ambapo alisema wanarahisisha biashara kwa kupakua mizigo inayoingia na kupakia inayosafirishwa nje hivyo huduma zao zinaathiri moja kwa moja maisha ya wananchi zinapokuwa bora zile bidha zinazopakulia mwisho gharama zikiwa kubwa za Bandari zinakwenda kuwaathiri wananchi.

Alisema kwenye maonyesho hayo watawaeleza kwamba bandari ya Tanga inafanya nini katika kurahisisha biashara na watawaeleza wananchi wa Tanga Bandari inafanya nini katika kurahiisisha biashara na kuongeza thamani ya ubora wa huduma.

Alisema ubora wa huduma ambazo zinatolewa lazima kuwe na vitendea kazi vya kutosha na bora kwa kuhakikisha meli inapokuja Bandarini lazima ikae muda mfupi kwa sababu ikikaa muda mrefu inaonyesha kwamba hiyo Bandari haina ufanisi.

Alisema kipimo cha Bandari yoyote Duniani ni ufanisi na kiasi gani mzigo unapakulia kwa saa na kiasi gani cha muda unamuhudumia mteja anapokuja kufuata huduma bandarini.

“Lakini unaweza kushindwa kutoa huduma bora kama vifaa ulivyonavyo vinaharibika mara kwa mara na hivyo kujikuta ukishindwa kufikia malengo uliojiwekea”Alisema

Hata hivyo alisema katika mwaka uliopita 2019/2020 walihudumia tani 569270 za shehena na mwaka huu ndani ya miezi sita wamehudumia tani 349205 na hivi sasa wameanza kupata shehena inayosafirishwa kwenda nchi jirani inayotumika kutengeneza saruji.




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini