BENKI YA CRDB YAPONGEZWA KWA KUANDAA PROGRAMU MAALUM YA KUIMARISHA AFYA | ZamotoHabari.

 Na Mwaandishi Wetu Mtwara

MKUU wa Wilaya ya Masasi Seleman Mzee ameupongeza uongozi wa Benki ya CRDB nchini kwa kuandaa programu maalum kwa ajili ya kuwezesha wafanyakazi wake kufanya mazoezi ya viungo kuimarisha afya zao.

Seleman Mzee ametoa pongezi hizo wakati akifungua hafla ya programu hiyo kufanya mazoezi kwa wafanyakazi wa CRDB Kanda ya Kusini yaliyofanyika wilayani Masasi.

Amesema hatua hiyo ni nzuri na CRDB wanapaswa kuendeleza mpango huo na kuwa endelevu huku akitoa rai kwa  taasis nyingine nchini zikiwemo za serikali kuiga huo mfano wa CRDB ili kuwapa nafasi wafanyakazi kufanya mazoezi na kuimarisha afya zao.

“Hili ni jambo la muhimu sana kwa ajili ya afya zetu, ni jambo ambalo hata katika ilani ya Uchaguzi ya CCM sura ya tisa, ibara ya 236 na 242, zinazungumzia afya, michezo kuptia michezo, Sanaa na utamaduni, eneo la michezo ndio moja wapo kama hii mnayofanya hapa,” amesema.

Amesema licha ya michezo kusaidia katika kuimarisha afya, Mzee amesema michezo pia huwaleta wafanyakazi pamoja, kufurahia na kudumisha uzalendo na mshikamano sehemu za kazi.

Kwa pande mwingine, Mzee amewaomba wafanyakazi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao kila mara ili kupata ushauri wa kulinda na kuimarisha afya zao.

Akiongea katika hafla hiyo Meneja wa CRDB Kanda ya Kusini Dennis Moleka amesema programu hiyo ya kufanya mazoezi kwa CRDB imeandaliwa na CRDB nchi nzima kupitia kanda zote na kwamba lengo ni kusaidia wafanyakazi kubadilisha staili za maisha ambayo wamezoea kuishi ili kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kuwakumba wafanyakazi hao kazini.

Amesema wafanyakazi wao hufanya kazi katika mazingira ambayo yapo ni magumu kufanya mazoezi kila mara na kwamba progamu hiyo itawasaidia kubadilisha ‘lifestyle’ ya maisha hayo kupitia michezo ambapo pia watapa wasaa wa kupima afya zao kila mara.


Mkuu wa Wilaya ya Masasi Seleman Mzee akipima urefu Kwa wataalamu wa afya katika uwanja wa mazoezi Masasi ikiwa ni sehemu ya Mpango wa CRDB uliyoandaliwa wafanyakazi wao kufanya mazoezi ya kucheza, kukkimbia ili kuimarisha Afya zao..
Wafanyakazi wa CRDB Kanda ya Kusini wakifanya mazoezi katika uwanja wa mazoezi Wilayani Masasi siku ya Jumapili iliyopita.


Maonyesho ya baadhi ya vyakula ambavyo wafanyakazi wa CRDB wanatakiwa kuvitumia katika Milo Yao ili kuimarisha afya

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini