KIWANDA KIKUBWA CHA MBOLEA KUJENGWA DODOMA, WATU 3,000 KUNUFAIKA ZA AJIRA YA KUDUMU | ZamotoHabari.


Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Kati Nchini (TIC), Aboubakari Ndwata akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli zinazoendelea katika Ujenzi wa kiwanda cha mbolea kutoka Kampuni ya Intrracom.
Mhandisi wa mradi huo wa kiwanda cha Mbolea, Tumaini Chonya kutoka Shirika la Umeme Tanesco akizungumzia hatua ambayo mradi huo umefikia.


Charles James, Michuzi TV

KIWANDA kikubwa Cha Mbolea kutoka kampuni ya intracom ya Nchini Burundi kinatarajiwa kujengwa Dodoma eneo la Nala ambapo Jumla ya watu 3000 watapata ajira za kudumu.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Meneja wa Kituo cha uwekezaji kanda ya kati ya Tanzania, Investment Center (TIC) Aboubakari  Ndwata katika Ziara ya kukagua shughuli zinazoendelea  kiwandani hapo.

Amesema kiwanda hicho ni kikubwa na kitakuwa na uwezo wa kutoa tani laki tano  za mbolea kwa mwaka.

" Kama tunavyojua tunaagiza mbolea nje karibu tani laki saba hivyo kiwanda hiki katika eneo la Nala kitakuja kuokoa pesa zetu hapa Nchini" Amesema Ndwata.

Amesema uwekezaji huo ni wa dola za kimarekani Bilioni 180 ambapo kwa Tanzania Ina thamani ya shilingi karibu Bilioni 400.

"Nachukua nafasi hii kumshukuru Rais wetu  Samia Suluhu Hassan baada ya kusema Serikali na Taasisi zake kuboresha fursa za uwekezaji.

Nawashukuru watoa huduma wa serikali ambao wamewezesha   kama tulivyoona nguzo zimetandazwa kilometa Tano kutoka chanzo Cha umeme lakini Shirika la umeme Tanzania limewezesha kuhakikisha umeme umefika" Amesema Ndwata.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa wawekezaji wengine ambao wana maeneo Nala kwenda kuanzisha viwanda kwani umeme na Maji yanapatikana muda wote.

"Eneo hili kulikuwa na shida ya umeme na Maji ilikuwa ukimleta muwekezaji  huku alikuwa anasema eneo ni porini hivyo shida ya umeme wala maji haipo wawaekezaji wote wenye maeneo waje kufungua viwanda" amesema Ndwata

Naye Mhandisi wa Mradi huo Tumaini  Chonya kutoka Shirika la umeme Tanesco Dodoma amesema mradi huo upo katika hatua ya Mwisho ya kukamilisha ambapo transformer   Yenye ukubwa  wa KVA 500 na nyingine KVA 50 imepita kwenye maeneo ya wananchi Ili waweze kupata umeme.

"Muda sio mrefu laini zote zitakuwa na umeme hapa naweza kusema asilimia  95 za umeme zimekamilika na hadi kufikia kesho kutwa umeme utakuwa umewaka kwa asilimia 100 "

Kwa Upande wake Mhandisi  Musafiri Deudonne  muwekezaji kutoka itracom kutoka nchini Burundi ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwa na kasi ya katika kuhakikisha miundo mbinu inakuwa rafiki katika utendaji Kazi.

Deudonne ameipongeza TIC na Serikali na wadau wengine waliowezesha kufanikisha umeme na Maji vinapatikana katika eneo la Nala kwani hiyo ndio ilikuwa changamoto kubwa kwa wawekezaji.

"Kasi imeonekana na Sisi itracom yunaahidi kuanzia wiki ijayo tutakuwa tumeanza mradi wetu wa Ujenzi wa kampuni ya mbolea  lakini pia yunaahidi kuanzisha miradi mingine Mingi"amesema Deudonne.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini