Majambazi Waliovamia Masista na Kuwafanyia Kitu Mbaya Wakamatwa Pwani | ZamotoHabari.

 


Jeshi la Polisi mkoani Pwani limewakamata watu tisa, akiwemo mwanamke mmoja, kati ya  watuhumiwa 12 wanaodaiwa kuwavamia na kuwajeruhi watawa watatu wa Kanisa Katoliki katika makazi yao, Ngoiga Vikuge wilayani Kibaha.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amesema leo Juni 4  kuwa watuhimiwa hao wanaendelea kuhojiwa huku wenzao wengine watatu wakiendelea kutafutwa.

Wankyo amesema watuhumiwa hao, May 31 usiku wakiwa na marungu, bisibisi na silaha zingine  walivamia nyumba wanayoishi watawa hao na kuvunja milango na wakawajeruhi watawa watatu.

Mbali na kuwajeruhi, walipora mali kadhaa zikiwemo fedha Sh2.5 mililioni, kompyuta mpakato mbili, simu mbili janja, kikombe maalumu cha ibada (ciborium) chenye ekarist, nguo na viatu mbalimbali.

“Katika tukio hilo, vibaka hawa walipambana na watawa hao na kuwajeruhi huku mmoja akichomwa na bisibisi usoni, na wameshapatiwa matibabu wanaendelea vizuri,” Wankyo.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini