Mambegu wakamilisha ujenzi wa zahanati,CCM wakoshwa na usimamizi wake | ZamotoHabari.

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wa kijiji cha Mambegu kata Luduga wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe,wanatarajia kuanza kupata huduma za matibabu katika maeneo ya karibu na kijiji chao kutokana na kukamilisha ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji hicho lililoghalimu  takribani milioni 124.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Mambegu mbele ya sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi iliyofika katika wilaya hiyo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani,diwani wa kata ya Luduga Hassan Ngela amesema.Wanachi wanatarajia kuanza kunufaika na upatikanaji wa huduma katika zahanati hiyo ikiwa ni ndoto yao ya muda mrefu na kuanza ujenzi mwaka 2019 kwa nguvu zao pamoja na wadau mbali mbali akiwemo mbunge na serikali.

“Tunashukuru sana serikali pia kwa tupatia milioni 50 ambapo zitamalizia kila kitu katika jengo hili na itabaki milioni mbili ambazo zitatumika kwenye ujenzi wa choo cha nje”alisema Hassan Ngela

Mwenyekiti wa kijiji cha Mambegu Keneth Msigwa amesema kukamilika kwa zahanati hiyo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwao hasa upande wa wanawake na wazee kwa kuwa huduma walikuwa wakifuata zaidi ya kilomita tano.

“Itasaidia sana ikishakamilika na tumemuomba mbunge atufanyie usajili kwasababu sasa hivi kinachokamilishwa ni umeme maji na milango”alisema Keneth Msigwa

Stephano Kinyangasi ni mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Wanging’ombe amewashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa ushirikiano wao na kusababisha kukamilika ujenzi wa zahanati hiyo huku akitaka vijiji vingine kuiga mfano wa kijiji hicho.

“Fedha za kutoka nje zimekuja kusapoti wakati wanakaribia kumaliza,sehemu zote wangeiga mfano wa mambegu tungekwenda mabli sana na tunawaomba wengine pia watangulize nguvu zoa na serikali itukute tukiendelea”alisema mwenyekiti wa CCM

Naye katibu wa CCM mkoa wa Njombe Amina imbo aliyefika na timu ya sekretarieti kwa ajili ya kukagua mradi huo amewashuuru viongozi na serikali kuendelea na utekelezaji wa ilani katika kukamilisha zahanati hiyo huku akiridhisha na jingo hilo.

“Tunashukuru sana kwa kukamilisha hili jingo kwasababu kuna majengo mengine yanakaa kwa muda mrefu lakini hapa wamesimamia vizuri na jingo limekamilika”alisema Amina Imbo

Viongozi wa Sekretarieti ya chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe akiwemo Amina Imbo katibu wa CCM mkoa wa Njombe,Amos Kusakula katibu wa jumuiya ya umoja wa vijana UVCCM,Erasto Ngole katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe,Frola Kapalie katibu wa UWT  Njombe na Agatha Lubuva katibu wa jumuiya ya wazazi wanaendelea na ziara mkoani Njombe kwa ajili ya kukagua uhai wa chama na Jumuiya zake,kukagua utekelezaji wa ilani pamoja na utekelezaji wa maagizo mbali kutoka ngazi ya juu ya chama.

Muonekano wa jengo la zahanati ya Mambegu kwa upande wa mbele likionyesha namna ukamilishwaji wake unavyoendelea ili kuanza kuwanufaisha wakazi wa kijiji hicho kwa kutoa huduma
Katibu wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Amina Imbo akifunguliwa moja ya chumba alipofika na kukagua jingo hili katika ziara yake ya kawaida kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo.
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi pamoja na viongozi wa sekretarieti ya mkoa wakiwa katika ukaguzi wa jengo la zahanati ya kijiji cha Mambegu.


 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini