MEYA SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MTAMBO WA KUCHAKATA TOPE KINYESI | ZamotoHabari.

 

Mhandisi Hezron Magambo kutoka SNV akielezea kuhusu Mtambo wa kuchakata tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (WASH SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi
***

Na Josephine Charles & Kadama Malunde - Shinyanga
Na Josephine Charles & Kadama Malunde - Shinyanga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila ameweka jiwe la msingi katika Mtambo wa Kuchakata Tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (Wash SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi kwa gharama zaidi ya shilingi milioni 290.

Akiweka jiwe la msingi la mtambo huo ,leo Alhamisi Juni 3,2021 katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga,  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. David Nkulila amesema tayari wamekamilisha kwa asilimia kubwa ujenzi wa mtambo  huo wa kisasa wenye mfumo wa kuchakata tope kinyesi na maji taka ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara na miundombinu ya mfumo ya maji safi na salama yenye lengo la kutokomeza magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu na homa ya matumbo.

Nkulila amesema mradi huo utasaidia kuyaweka mazingira ya Manispaa ya Shinyanga katika hali ya usafi ambapo utasaidia pia ule Mpango wa Manispaa ya Shinyanga kuwa Jiji kwa sababu maji taka yote yatakuwa yanaletwa katika eneo hilo.

“Lakini pia Kupitia Mradi huu baada ya tope kinyesi kuchakatwa yale maji yatafaa kufugia samaki na tunatarajia kuwa na mradi wa kufuga samaki hapa. Hivyo Manispaa ya Shinyanga tutakuwa na Mradi wa Samaki pia Kupitia Mradi huu”,amesema Nkulila.

Nkulila ameliomba Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) liendelee kuleta miradi kwa ajili ya maendeleo ya nchi hasa Manispaa ya Shinyanga.

Nkulila amewataka Watendaji wa Manispaa ya Shinyanga na Idara zinazohusika na wananchi kwa ujumla kuutunza mradi huo na huku akiliahidi Shirika hilo kupitia kwa Meneja Mradi huo Bwana Olivier Germain kuwa watautunza na itakuwa ni sehemu ya utalii wa ndani kwa Manispaa ya Shinyanga.

Awali akisoma  taarifa ya mradi huo, Mhandisi Hezron Magambo kutoka SNV amesema mradi huo ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2017 na utakamilika mwaka 2022 ambapo utasaidia kuboresha upatikanaji na utumiaji wa huduma za usafi wa mazingira na kuboresha tabia ya usafi.

Amesema huo umelenga tabia mbalimbali zikiwemo utupaji hovyo wa taka ngumu kwenye mashimo ya vyoo ikiwemo taulo za kike, watu kutokuwa na chombo maalum cha kuhifadhia taka, unawaji wa mikono nyakati zote muhimu na kunyonya tope kinyesi kwa wakati kabla ya choo hakijafurika.

Amesema endapo watu wataacha tabia mbaya za usafi wa mazingira, jamii itabaki kuwa salama kiafya ,itaepukana na magonjwa ya Mlipuko kama Kipindupindu.

Meneja mradi wa Shirika la SNV la Uholanzi Bwana Olivier Germain amesema mtambo huo utasaidia kutokomeza magonjwa ya mlipuko na kusaidia kuzalisha nishati mbadala pamoja na mbolea Kwa ajili ya kilimo.

Aidha amepongeza Uongozi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kuupokea Mradi na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kuutekeleza huku akimshukuru aliyekuwa Mkurugenzi wa SHUWASA marehemu Flaviana Kifizi kwa kujitoa kwake katika utekelezaji wa mradi huo enzi za uhai wake na amemuombea aendelee kupumzika kwa amani huku pia akiwapongeza wafanyakazi wa SNV kwa kujitoa kwao katika Mradi huo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi amesema Manispaa ya Shinyanga imebahatika kujengewa Mradi ambao ni wa kipekee Tanzania nzima, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuutunza ili waendelee kuletewa miradi mingine.

“Tukifanya kwa vitendo, malengo ya Kampeni hii ya Mazingira Safi Maisha Bora ni kweli maisha yetu yatakuwa bora na afya zitaimarika”,ameongeza Mwangulumbi.

Mwenyekiti wa bodi Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Bi. Mwamvua Jirumbi amepongeza kukamilika kwa mradi huo akibainisha kuwa upo umuhimu wa kuendelea kushirikiana na mamlaka zingine za serikali na wadau kujenga miradi ya kimkakati kama huo.

Mradi wa usafi wa Mazingira WASH SDG unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo Uholanzi  (SNV) na umebeba kauli mbiu ya tabia bora za usafi wa Mazingira inayosema 'Mazingira Safi Maisha Bora' kwa Tanzania unatekelezwa katika miji miwili ya Manispaa ya Shinyanga na Jiji la Arusha.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. David Nkulila akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la Msingi Mradi wa Kuchakata Tope Kinyesi ambao umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Uholanzi(SNV) Kupitia WASH SDG PROG. kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)  uliojengwa katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geofrey Mwangulumbi akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la Msingi Mradi wa Kuchakata Tope Kinyesi ambao umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Uholanzi(SNV) Kupitia WASH SDG PROG. kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)  uliojengwa katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga 
Meneja Miradi wa Shirika la SNV la Uholanzi Bwana Olivier Germain akielezea kuhusu Mtambo wa Kuchakata Tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (Wash SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi
Mwenyekiti wa bodi Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) bi. Mwamvua Jirumbi akizungumza
Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. David Nkulila akiweka jiwe la Msingi Mradi wa Kuchakata Tope Kinyesi ambao umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Uholanzi(SNV) Kupitia WASH SDG PROG. kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)  uliojengwa katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga 
Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. David Nkulila akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kuchakata Tope Kinyesi ambao umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Uholanzi(SNV) Kupitia WASH SDG PROG. kwa Kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)  uliojengwa katika kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Mkoa wa Shinyanga 
Mhandisi Hezron Magambo kutoka SNV akielezea kuhusu Mtambo wa Kuchakata Tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (Wash SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi
Mhandisi Hezron Magambo kutoka SNV akielezea kuhusu Mtambo wa Kuchakata Tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (Wash SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi

Mshauri wa Mradi kutoka  Edge Engeneering and Concult Ltd, Deus Nshange akielezea Kampuni yao jinsi wanavyoshirikiana na SNV,SHUWASA na Manispaa ya Shinyanga kuutekeleza Mradi huo wa Unyonyaji Tope Kinyesi
Sehemu ya Mtambo wa Kuchakata Tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (Wash SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi
Gari la majitaka likiwa kwenye eneo la mradi
Muonekano wa Mtambo wa Kuchakata Tope Kinyesi uliojengwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV – Netherlands Development Organization) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kupitia Mradi wa Usafi wa Mazingira (Wash SDG) na kufadhiliwa na Serikali ya Uholanzi


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini