Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameishauri Wizara ya Maliasili na Utalii kupunguza utitiri wa Kodi zilizopo ambazo zimekuwa kikwazo kwa waendesha watalii nchini.
Aidha, ameishauri Wizara kukaa nao pamoja Ili kuzungumza na kuweza kujua changamoto walizonazo na mahitaji yaliyopo katika sekta ya utalii.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2021/2022,Juni 5 bungeni,Mtaturu amesema kuna kampuni binafsi zinazotembeza watalii wanafanya kazi nzuri kwa niaba ya serikali na wao ndio wanakutana na watalii moja kwa moja hivyo ni vyema wakapewa nafasi ya kusikilizwa ili kueleza changamoto na mahitaji ya watalii.
“”Lazima tujue watalii wetu wanataka nini cha kuwavutia zaidi,tusiwe tunaweka vitu kwa utashi wetu hii itakuwa ni sawa sawa na muuza duka kuuza nguo ya style fulani anazozipenda yeye badala ya kutafuta nguo wanazozipenda wateja,Niwaombe mkae na Tour Operators waweze kuwaambia taste ya watalii ikoje na wanataka nini,
Akizungumzia kuhusu utitiri wa Kodi na tozo amesema,”Katika sekta hii kuna tozo 20 ambazo zimekuwa kikwazo,ni vizuri zikaangaliwa upya,tunajua Kodi inasaidia kuboresha maisha ya wananchi lakini ni vizuri walipe Kodi kwa furaha ili Kodi hiyo iwe endelevu,”aliongeza.
Ameishauri pia Wizara kutangaza vivutio vilivyopo katika mikutano mbalimbali Duniani ikiwemo World Travel Market (WTM),ili kusaidia Utalii uweze kutangazika duniani kote.
” Niipongeze Wizara inafanya kazi nzuri na bajeti yenu imeonyesha Mpango mzuri na tunapotoa ushauri hapa ni kwamba tunataka tuendelee kuwa na uhakika wa Mapato ili kusaidia nchi katika maendeleo,
Amefafanua kuwa,”Tunafahamu wizara hii inaongoza kuiletea nchi mapato,asilimia 17 ya Pato la Taifa na asilimia 25 ya fedha zote za kigeni ni nyingi na zinaimarisha serikali katika kutoa huduma ya maendeleo kwa wananchi,lakini pia sekta hii inazalisha ajira Mil 1.6, kwa kweli tukifanikiwa kuondoa vikwazo nilivyovitaja tutaongeza tija na kuvutia watalii zaidi na hivyo lengo la wizara kufikia watalii Mil 5 litafikiwa,”alisisitiza.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments