Hakuna shaka kwamba msanii nguli wa nyimbo za injili, Rose Muhando, ndiye malkia na gwiji wa nyimbo za injili Afrika Mashariki na Kati. Msaanii huyu alianza kuvuma kwa muda mrefu sana na kiwango chake kimebakia juu pamoja na kwamba umri wake kwa sasa umesogea. Album kali kabisa ya Rose Muhando nilianza kuisikia mwaka 2008 lakini kabla ya hapo naambiwa alikwishatoa album moja matata sana (ambayo nadhani ndio ilikuwa album ya kwanza). Na tangu nimfahamu sijawahi kuchoka kusikiliza nyimbo zake zenye upako:
Pamoja na umaarufu wa Rose, siku za karibuni ilionekana kama vile afya yake imetetereka na akawa kimya kwa muda bila kuingia studio kufyatua vibao vipya. Kwa mara ya kwanza nilimuona akiombewa na mchungaji mmoja kutoka huko Kenya na kweli afya yake haikuwa sawa:
Baada ya tukio lile baadhi ya watanzania wasiomtakia mazuri walianza kumzushia uzushi wa hapa na pale ilimradi kila mtu alisema lake. Wengine walisema yupo hoi taabani anaumwa na hata kumzushia kuwa anasumbuliwa na majini. Sio vizuri ndugu zangu. Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako (Luka 6:41-45).
Mbaya zaidi, watu wengine wakamzushia kifo. Mmoja wa watanzania hawo wasiomtakia mema ni ndugu anayemtaja kwenye video hapa chini. Ukweli ni kwamba Rose sasa ameimarika kiafya na anaendelea kuihubiri injili ya Bwana wetu Yesu Kristo kuptitia uimbaji kama anavyokiri mwenyewe (sikiliza video). Tuache uzushi ndugu zangu, sio kitu kizuri:
Kinachoniuma ni kuwa, baada ya Rose kupata misukosuko ya kiafya, nilitarajia watanzania wawe wa kwanza kumtakia mema kiuzalendo zaidi lakini wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kumnyali mitandaoni na kumtamkia maneno mbofumbofu. Hata wachungaji wa kitanzania nao hawakwepi lawama hizi kwani walishindwa kumuombea hadi ikabidi aende kuombewa nchini Kenya. Hii ni ishara mbaya sana kwa watanzania na ni kiashiria cha kuporomoka kwa uzalendo na umoja wa kitaifa tulioachiwa na mwasisi wa taifa hili, hayati Julius Kambarage Nyerere. Watanzania tunakwama wapi hasa? Kwanini hatupendani? Uzalendo na utaifa aliotuachia baba wa taifa umepotelea wapi?
Kitendo cha watanzania kumshit Rose ni kama vile waliamua kumtelekeza porini akaokotwa na wasamalia wema (Wakenya). Kama shukrani zake kwa wakenya waliomuokota baada ya kutupwa porini, Rose ametunga kibao hiki hapa kuisifu na kuiombea serikali ya Kenya kwa sababu ya watu wake kumpa sapoti ya kutosha:
Kama nilivyotangulia kusema, Rose ni mwanamuziki nguli na ni deal kubwa kwa promoter yeyote wa muziki anayejua kutumia vizuri vipaji vya wasanii. Hapa Tanzania kuna mtu mmoja anaitwa Alex Masama anayewapromote wanamuziki wa nyimbo za injili. Namulaumu sana kwa kumuacha Rose aende kujenga uchumi wa wakenya badala ya kumzuia abakie hapa hapa nchini. Ama kweli nabii hakubaliki kwao. Wakenya sasa hivi wanapiga hela ndefu mno kupitia Rose. Tazama jinsi anavyokusanya mtiti wakenya wanagema sadaka wanajenga uchumi wa nchi yao:
Uzembe wa watanzania kama huu tulioufanya kwa Rose ndio umepelekea wakenya wajitangazie kuwa Mlima Kilimnjaro upo kwao na sisi tumekaa kimya. Hatujui kuchangamkia fursa ndio maana tunaonekana vilaza hadi kumtelekeza msanii nguli akaokotwa na wakenya. Sisi tumekalia majungu na kutakiana mabaya badala ya kunyanyuana kama ndugu. Shame on us!
Watanzania ni shida sana hasa kwenye suala la kunyanyuana kwa hali na mali. Ifike mahali watanzania tujenge utamaduni wa kupendana na kusapotiana kwa kila jambo jema kwa maslahi mapana ya taifa letu. Kitendo cha kinyama alichofanyiwa Rose Muhando hakitaiacha nchi hii salama.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments