Na Hamida Kamchalla, TANGA.
WAJASIRIAMALI wanaotaka kupata huduma za Shirika la Viwango nchini (Tbs) kama cheti cha ubora wa viwango wameshauriwa kufuata njia sahihi ya kupatiwa mafunzo na Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO) ambayo itawarahisishia kupata huduma hizo bure bila gharama yoyote.
Akiongea katika maonyesho ya nane ya biashara mkoani Tanga, Mkurugenzi mkuu wa Shirika la viwango nchini (Tbs) Athumani Ngenya alisema endapo mjasiriamali atafuata njia hiyo atapatiwa huduma za Tbs bure kwa muda wa miaka mitatu.
"Wale wote wanaofanya shuhuli za ujasiriamali wanaohitaji kupata nembo za Tbs, njia ya kufanya ni kwenda kwanza SIDO kule watapatiwa mafunzo kwa bidhaa wanazotengeneza kisha watapewa vyetu ambavyo vitawaruhusu wao kukamilisha kupata huduma zetu, sisi tunafanya kazi laribu źidi na SIDO" alisema Ngenya.
"Lakini kabla hawajakuja kwetu ni lazima wapewe barua ya kuwatambua kutoka huko SIDO na hapo sisi tutawatambia na kuwapatia huduma za zetu kwa gharama sifuri, kwa maana gharama zile zinalipwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania" aliongeza.
Aidha Ngenya alifafanua kwamba katika maonyesho hayo, mbali na kutangaza huduma zao pia wanatoa elimu kwa wananchi hasa wale wanafika kutaka huduma za Tbs kama wale wauzaji wa nidhaa za vyakula na vipodozi ambao wanahitaji kupata usajili wa nembo yetu katika bidhaa zao.
Ngenya alibainisha kuwepo kwa bidhaa nyingi zisizokuwa na ubora hasa katika vifaa vya ujenzi, umeme, nguo na hata vyakula ambavyo wanajitahidi kuvitambua na kuviondoa kabisa sokoni huku akitoa wito kwa wananchi kutotumia bidhaa zisizofaa na endapo watazibaini watoe taarifa Tbs nao watachukua hatua stahiki kwa muuzaji atakapobainika ana hatia.
"Madhara ya kutumia bidhaa ambazo hazikuthibitishwa kama vya umeme yako wazi, kwanza vinaweza kupata joto kwa muda mfupi na hatimaye kuungua na pia zinaweza kusababisha hasara ya kuunguza vitu vingine vitakavyokuwa karibu na eneo la tukio" alieleza.
"Nataka nitoe wito kwa Watanzania kuacha kutumia bidhaa feki, katika kuzitambua bidhaa hizo mteja anaponunua kwanza anapaswa kuangalia nembo ya Tbs kwa bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini, lakini hata zile zinazotoka nje pia unaweza kumuuliza muuzaji, akikuthibitishia imethibitishwa na ikitokea siyo kweli hatua zitachukuliwa dhidi yake" alibainisha.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments