Barbara Gonzalez ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Simba SC, amezaliwa Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita, baba yake akiwa ni raia wa Colombia na Mama Mtanzania, mbali kuwa msaidizi wa Mohamed Dewji, pia ni aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mohamed Foundation aliyojiunga nayo Aprili, 2016 ambayo imekuwa ikitoa msaada wa huduma za kijamii kwa makundi mbalimbali nchini.
-
Pia anahudumu katika Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Young African Leaders Initiative (YALI) iliyo chini ya Rais wa zamani wa Marekani, Barrack Obama ambayo lengo lake kuu ni kuwekeza katika viongozi wa kizazi cha baadaye barani Afrika.
-
Mbali na wadhifa huo, Barbara pia ni mshauri wa taasisi ya Deloitte Consulting Limited Tanzania na pamoja na hilo, amefanya kazi katika miradi kadhaa iliyo chini ya mashirika makubwa duniani miongoni mwao yakiwa ni USAID, UNICEF, Benki ya Dunia na Plan International.
-
Mwanadada huyo ana uzoefu wa kutosha na ni mbobezi wa masuala ya utawala na uongozi akiwa na Shahada ya Uzamili ya Utawala na Maendeleo aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Uchumi na Sayansi ya Siasa kilichopo London, England.
-
Alipata shahada yake ya kwanza aliipata katika Chuo Kikuu cha Manhattanville College kilichopo New York, Marekani ambako alihitimu kwa ufaulu wa juu katika Sayansi ya Siasa na Uchumi.
-
#JICHOLAUSWAZI
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments