ZINGATIA HAYA KWA WENYE MAGARI YA ‘AUTOMATIC’
Usiweke ‘Neutral’ mteremkoni, hii inazuia Oil kusambaa na kusababisha msuguano kwa kukosa kilainishi hicho na kupelekea kusagika kwa baadhi ya sehemu. Usiwashe gari na kuanza kuvuta mafuta hii husababisha msuguano mkali na unaweza kuharibu sehemu za Injini
Usiweke ‘Neutral’ unapokuwa kwenye taa za barabarani, watu wengi hufanya hivyo ili kuhifadhi mafuta lakini kiasi unachohifadhi ni kidogo sana kulinganisha na gharama ya tatizo unaloweza tengeneza
Usiweke ‘Parking’ kabla gari halijasimama kabisa. Hakikisha gari limesimama kabisa ndipo unaweka ‘Parking’. Usiendeshe gari kwa kasi kabla Injini kupata joto, hakikisha injini imepata joto ili kuwezesha ‘Oil’ kusambaa kwenye sehemu zote
Kuacha mafuta machache kwenye ‘Tank’ unapolipumzisha gari lako, ‘Tank’ la mafuta linatakiwa kuwa limejaa au kuwa nusu lakini sio chini kabisa. Kujaza mafuta kunasaidia injini na sehemu nyingine kupoa
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments