Oktoba 1993 hali ya Joshua ilikuwa wa leo wa kesho! Wazazi wa Joshua, Abdul-Hakim na Diane Torres, walitamani kumfanyia kitu mtoto wao ili atabasamu kabla ya kifo.
Walimuuliza nini wamfanyie? Akajibu angependa kuonana na Tupac au kuzungumza naye kwa simu. Tupac alikuwa maarufu na tajiri. Mamilioni walitamani kukutana naye. Mwaka huo ndio albamu yake "Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z" ilikuwa inakimbiza sokoni. Wangemfikiaje?
Wakamwambia atoe ombi lingine. Akataja mastaa wanne. Wazazi wa Joshua walienda kwenye taasisi ya kufanikisha ndoto, Make A Wish Foundation iwasaidie kumuunganisha Joshua na Tupac au mastaa wengine waliotajwa. Taasisi hiyo iliwakatalia.
Waliishi Aberdeen, Maryland. Oktoba 14, 1993, Diane (mama wa Joshua) alipiga simu kituo cha Redio WPGC, Washington DC kuomba msaada. WPGC walirusha tangazo kuhusu kiu ya Joshua.
Baada ya tangazo, zilipita dakika 30, Diane alipokea simu ya Tupac. Machozi yalimtoka kwa furaha, akamfuata Joshua aliyekuwa amelala kitandani, akamwambia: "Josh, ongea na Tupac." Joshua kusikia Tupac moyo ukalia pah! Akapata nguvu ghafla.
Joshua na Tupac waliongea kwa saa nzima. Tupac akamuuliza Joshua amfanyie nini zaidi? Joshua akaomba amtembelee amuone. Tupac alikuwa New York, kufika Aberdeen kwa haraka ilihitaji ndege. Na story aliyopewa ni kuwa Joshua asingeweza kuamka siku iliyofuata.
Tupac akachukua walinzi na wasaidizi wake, akakodi ndege. Usiku saa 2 alikuwa Aberdeen amekumbatiana na Joshua. Walilia na kuimba pamoja. Joshua alirap wimbo mzima "Keep Ya Head Up" wa Tupac. Tupac alimpeleka Joshua uwanja wa Baseball kungalia mechi. Saa 5 usiku Tupac alipanda ndege kurejea New York.
Alipofika New York, baba wa Joshua alimpigia simu Tupac kumweleza kuwa Joshua tayari ameshachukuliwa na Mungu. Akamshukuru kwa kumpa tabasamu kabla ya kifo. Tupac akabadili jina la kampuni yake ya Ghetto Gospel kuwa Joshua's Dream.
By Luqman
SOMA MAKALA HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments