Profesa Lipumba apata chanjo ya Covid-19 | ZamotoHabari.



Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amepata chanjo ya kwanza ya kujikinga na ugonjwa wa corona.
Profesa Lipumba amepata chanjo hiyo leo Jumatano Julai 22,2021 katika kliniki ya Umoja wa Mataifa zilizopo Masaki.

Akizungumza na waandishi baada ya kutoka kupata chanjo hiyo amesema amejikuta akipata nafasi hiyo kupitia mke wake, Gojina Mtenga, anayefanya kazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto Duniani(Unicef), Cox Bazaar nchini Bangladesh.

"Kama mlivyosikia wenzetu wa mashirika haya ya kimataifa wameruhusiwa kuanza kupata chanjo hizi pamoja na familia zao.

"Hivyo na mimi kupitia mke wangu ndio imeniwezeaha leo kuja kupata chanjo hii hapa na nilipata taarifa usiku wa jana ikinitaka nifike hapa leo saa tano asubuhi nashukuru kwa kulikamisha hili, "amesema Profesa Lipumba.

Hata hivyo amesema baada ya chanjo hiyo  ya awali anatakiwa arudi tena baada ya wiki sita mpaka nane kupata chanjo ya pili ili kukamilisha chanjo nzima ya kujikinga ya kujikinga na ugonjwa huo.

Pia mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuchangamkia chanjo hiyo ili kuwa salama.

Wakati kwa upande wa Serikali ameishauri iangalie namna ambayo itawezesha wananchi wanaougua ugonjwa huo kupata matibabu kwa yake kwa gharama nafuu.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini