KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ amewaondoa hofu Wanayanga kwa kuwaambia kuwa aendi popote na ataendelea na timu hiyo katika msimu mwingine mmoja.
Kauli hiyo imewafurahisha mashabiki wa timu hiyo baada ya taarifa kuzagaa kuwa anaondoka mara baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba, wikiendi ijayo.
Mkongwe huyo juzi mara baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, alitupia ujumbe kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram uliotafsiriwa vibaya na mashabiki wa timu hiyo wakifahamu anaondoka.
Saido amesema, yeye bado ni mchezaji halali wa Yanga mwenye mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu hiyo.
Aliongeza kuwa, ana malengo makubwa na timu hiyo katika kuelekea msimu ujao na kikubwa anataka kuipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kama zawadi kwa mashabiki.
“Niwaondoehofu mashabiki wa Yanga kwa kuwaambia kuwa mimi bado nina mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuwa hapa.
“Hayo mengine yanayoendelea katika mitandao ya kijamii ni uzushi tu, mimi sijasema popote naondoka, hivyo waondoe hofu.
“Bado nina mengi ya kuwafanyia Yanga katika msimu ujao kati ya hayo ni ubingwa wa ligi,” alisema Saido.
Saido raia wa Burundi, alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu akiwa mchezaji huru, amefanikiwa kufunga mabao manne kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.
WILBERT MOLANDI | GPL
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments