Official Dj wa msanii Harmonize Dj Seven Worldwide kutoka Konde Gang Music amefunguka kutamani kufanya kazi na msanii Alikiba anayewakilisha lebo ya Kings Music Records.
Dj Seven amesema haoni tofauti kufanya kazi na msanii mwingine nje ya Konde Gang kwa sababu mziki ni biashara na yeye anatafuta kitu kitakacholeta faida.
"Kuna msanii ambaye anamiliki lebo nimemuomba kufanya naye kazi kama itakuwa poa tutafanya, nataka kufanya kazi na Alikiba tumeshaongea na Producer wake Yogo kila kitu kikiwa sawa tutafanya wimbo" ameeleza Dj Seven Worldwide
Mpaka sasa Dj huyo ameshafanya kazi na wasanii mbalimbali wa BongoFlava kama Young Lunya, Salmin Swaggz, Linah, Mimi Mars na Baddest.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments