Naibu Waziri aeleza Gereza lilivyoelemewa wafungwa | ZamotoHabari.

 


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geofrey Pinda, amesema kuwa gereza la Mpanda mkoani Katavi, limeelemewa na wafungwa kwani uwezo wake ni kubeba wafungwa 100 tu lakini hadi sasa lina jumla ya wafungwa 400.

Naibu Waziri Pinda ameongeza kuwa kufuatia hali serikali imejipanga kujenga magereza mawili ili kupunguza changamoto hiyo, ambapo mpaka sasa tayari maeneo yamekwishatengwa kwa ajili ya ujenzi wa magereza hayo.

Gereza la Mpanda mkoani humo limejengwa mwaka 1947.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini