DKT. SENGATI CHANJO NI BURE AONYA CHANJO YA UVICO 19 KUTOLEWA KWA FEDHA | ZamotoHabari.

Na Anthony Ishengoma -Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amewataka watoa huduma ya Chanjo ya Uvico 19 Mkoani Shinyanga kuwa waadilifu na wazalendo kwa kuzingatia haki katika zoezi zima la utoaji chanjo hiyo kwa walengwa wote. 

Dkt. Sengati alisistiza watoa huduma hao wa sekta ya Afya kuzingatia kuwa chanjo hiyo inatolewa bure na serikali nakuonya kuwa isije ikatokea mtu yeyote akatozwa fedha kwa jili ya kupatiwa huduma ya Chanjo ya Uvico 19.

Dkt. Sengati alisema hayo jana katika hotuba yake ya uzinduzi wa zoezi la chanjo ya Uvico 19 iliyozinduluiwa rasmi jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuongeza kuwa huduma ya chanjo hiyo itatolewa katika vituo vitatu kila vya kila Halmashauri ikiwemo hospital ya Mkoa wa Shinyanga.

‘’Uzinduzi wa chanjo hii katika mkoa wa Shinyanga unatoa fursa kwa wananchi waliotayari kuchanja na kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa pamoja na kupunguza hatari ya madhara makubwa endapo mtu atapata maambukizi.’’Dkt. Sengati aliendelea kusema.

Naye Mganga Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile alisema kuwa Mkoa wa Shinyanga umepokea dozi elfu 25 kwa ajili ya Mkoa wa Shinyanga ambazo zitasambazwa katika vituo 18 vilivyobainishwa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga.

Dkt. Ndungile alisema Ofisi yake imetenga vituo vitatu vitatu kwa Halmshauri sita za Mkoa wa Shinyanga na kufanya jumla ya vituo 18 mkoa mzima kutumika kwa ajili ya kutolea chanjo hiyo ambapo kila anayehitaji huduma hiyo atajisajili kwa njia ya mtandao ili kuweza kujipangia siku na tarehe ya kupatiwa chanjo hiyo.

Dkt. Ndugile aliongeza kuwa uchaguzi wa vituo hivyo umezingatia uwepo wa wataalamu wa chanjo katika vituo husika lakini pia jiografia ya kila Halmashauri ikiwemo uwezo wa kuwahudumia wananchi wa kawaida na wale wanaohitaji kupa chanjo hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Shinyanga Shekhe Hamisa Balulisa ameviambia vyombo vya habari kuwa chanjo hiyo ni salama kwa kuwa wataalamu pamoja na Serikali wametuaminisha kuwa chanjo hiyo ni salama na kuwataka wananchi kujitokeza kwa ajili ya chanjo hiyo na kusisitiza kuwa chanjo sio kosa kwa kuwa inakubalika katika imani.

Shekhe Balulisa ameongeza kuwa kuwa chanjo hii ni kwa ajili ya makundi maalum basi itakupaji chanjo kwa ajili ya makundi mengine basi wajitokeze kupata chanjo kwa ajili ya kinga kwa kuwa kinga hiyo kwani suala lakinga pia likubalika pia  katika masuala kiimani.

Chanjo ya Uviko 19 imezinduliwa jana Mkoani Shinyanga na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Philemon Sengati inatendelea katika vituo 18 katika vituo vitatu kwa kila Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga na zoezi hili linaendelea katika Mikoa yote Nchini baada ya Rais wa Tanzania Smaia Suluhu Hassan kuzindua zoezi hilo kitaifa hapa Nchini.  


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akisaini fomu ya hiari ya chanjo ya Uvico 19 mara baada ya kuzindua zoezi la chanjo hiyo kwa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akipata chanjo ya Uvico 19 mara baada ya kuzindua chanjo hiyo Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Mkude akichoma chanjo ya Uvico 19 kufuatia uzinduzi wa chanjo hiyo mkoani Shinyanga jana.
Muhasibu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Burton Mwakanyamala   akichoma chanjo ya Uvico 19 kufuatia uzinduzi wa chanjo hiyo mkoani Shinyanga jana.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini