"JANUARY MAKAMBA ATOA MSAADA WA VITANDA KWA WANAFUNZI VYENYE THAMAN YA Mil4" | ZamotoHabari.

 Walimu na Wanafunzi wa shule ya sekondari Soni day iliyopo Bumbuli Mkoani Tanga wamemshukuru Mbunge wao  January Makamba kwa kutimiza ahadi yake  ya vitanda 20 vyenye thamani ya mil.4.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi walisema 'hostel' ya shule yao iliungua mara mbili na tangu ikumbwe na kadhia hiyo walikumbana na changamoto ya ukosefu wa vitanda hivo kulazimika kulala chini kutokana na vitanda vilivyokuwepo kuungua wakati wajanga hapo shuleni kwao.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu aliyefahamika kwajina la  Mashoo Mrema alisema kuwa msaada huo wa Mbunge umekuja wakati muafaka wakati wao wakiwa na uhitaji wa vitanda hivyo.

Mrema alisema kuwa pia vitanda hivyo vitawasaidia kuwapa nguvu ya kujisomea na kuondokana na mawazo na magonjwa ya kukohoa waliyokuwa wanayapata kutokana na kulala chini.

Ally Lwena ni Mkuu wa shule hiyoAlisema Kwanza anampa shukrani Mbunge wao kwa Kusikia Kilio hicho Cha vitandanda  vya wanafunzi wa kike katika shule hiyo.

Lwena alisema hatua hiyo itasaidia kupata wanafunzi wengi watakaokaa Hostel na hivyo kuwaongezea Muda Mwingi Wakujisomea hatimaye Kuongeza Ufaulu wa Shule Na Halmashauri kwa Ujumla.

Pia Mkuu huyo wa shule alieleza kuwa kutokana na kukosekana kwa vitanda Wanafunzi walikuwa wakipigwa na baridi kali iliyokuwa inatoka kwenye sakafu na kuwapata moja kwa moja wanafunzi Ilisababisha magonjwa kama vile kukohoa , kubanwa na mbavu na hata vichomi.

Kwa upande wake Mbunge Makamba alisema tangu ameingia madarakani amekuwa akisadiana na  wananchi wake kutatua changamoto mbalimbali pamoja na kutekeleza ahadi anazoahidi.

Makamba alisema wakati shule hiyo imekumbwa na kadhia ya janga la moto yeye kama Mbunge alitoa fedha zake mfukoni na fedha kutoka kwa marafiki zake waliweza kununu vitanda 100 na bati 200 nakwamba ahadi iliyokuwa imebaki ni hiyo ya vitanda ambayo inakamilika Sasa.

Hata hivyo alieleza kuwa lengo la kusaidia katika shule hiyo ni kutaka kuunga mkono  jitihada za kuinua kiwango Cha elimu na ufaulu   katika jimbo lake.




APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini