HUU sasa ni uchokozi… Eti Ibraah naye anataka kujipumzisha kwa mzazi mwenza wa Rayvanny, Fahyma ili tu kuendeleza ligi kati ya wasanii hao wanaotoka katika lebo hasimu.
Ibrahim Abdallah almaarufu Ibraah anatokea katika lebo ya Konde Music World Wide iliyo chini ya Harmonize wakati Raymond Mwakyusa au Rayvanny anatokea kwenye lebo ya Wasafi ambayo ndiyo iliyompika Harmonize.
Kupitia ukurasa wake wa Insta story Ibraah ameposti picha ya Fahyma na kuandik Mama G, jambo ambalo limeibua mjadala mzito kwa mashabiki wa wasanii hao huku wengine wakidai kuwa Ibraah anataka kulipiza kisasi.
Hatua hiyo inakuja baada Rayvanny kumuacha Fahyma na kuangukia katika penzi la Paula Kajala mrembo ambaye pia Harmonize alitaka kujinyakulia lakini akadakwa na kisha kupigwa kibuti na mama mzazi wa binti huyo Kajala Masanja.
Ibraah na Rayvanny ni mahasimu kiasi cha kutungiana nyimbo za kutusiana huku sababu kubwa ikidaiwa kuwa ni mapenzi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments