Waziri Ummy aagiza ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Njombe uanze mara moja | ZamotoHabari.


Na Amiri Kilagalila,Njombe

 Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe, Ummy Mwalimu (MB) Amebariki Maamuzi ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ya Kutaka Makao Makuu ya Halmashauri Hiyo Kujengwa Katika Kijiji Cha Kidegembye Kata ya Kidegembye na Kuagiza Zoezi la Kuanza Ujenzi Lianze Haraka Iwezekanavyo.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo wakati akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa makao makuu ya  halmashauri hiyo na kujiridhisha kuto kuwepo kwa mgogoro wowote katika mchakato huo wa ujenzi

Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe,Afisa Uhusiano wa Halmashauri Hiyo Lukelo Mshaura Amesoma taarifa ya Mchakato wa Ujenzi wa Majengo ya Utawala Katika Halmashauri Hiyo Ambapo amesema Baadhi ya Fedha Zilizotolewa na Serikali Kwa ajili ya Ujenzi wa Makao Makuu Zilishanza Kutumika Hadi Walipositishwa Kuendelea.

"Kwenye kikao cha baraza la madiwani cha tarehe 6 mwezi wa nne 2020,kiliazimia makao makuu ya halmashauri yawe Kidegembye.Eneo hili ambalo linajengwa ofisi za halmashauri linakadiriwa kuwa na ekari 10 na katika bajeti ya mwaka 2020,2021 halmashauri iliidhinishwa fedha bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala na katika kipindi cha robo ya nne halmashauri ilipokea jumla ya shilingi milioni 900"alisema Mshaura

Tamko la Kuunga Mkono Maamuzi ya Madiwani Hao Amelitoa Akiwa Mtwango Baada ya Kuzulu Katika Kijiji Cha Kidegembye na Matembwe Ambako Imejengwa Hospitali ya Wilaya Ambapo Amesema Hakuna Sababu ya Kuendelea Kusubirisha Jambo Hilo Ilihali Serikali Ilishatoa Shilingi Milioni 900 Kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu Hayo na Kisha Kusitishwa Baada ya Kutolewa Maelekezo ya Maeneo Mawili Ya Kujenga Kati ya Kidegembye na Matembwe.

"Nakubariana na uamuzi wa madiwani makao makuu ya halmashauri yatajengwa Kidegembye,kwa hiyo Kidegembye ndio itakuwa makao makuu ya hallmashauri ya wilaya ya Njombe na ujenzi uanze kesho fedha milioni 940 zimekuja kesho nataka kuona watu site"alisema Ummy Mwalimu

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Valentino Hongoli Pamoja na Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Swale Amesisitiza Kutokuwapo Kwa Mgogoro Juu ya Eneo la Ujenzi wa Makao Makuu Hayo Huku Wakisema Wananchi wa Kidegembye Wamejitolea Kutoa Eneo Kubwa Kwa ajili ya Shughuli Hiyo.

"Wana Kidegembye walitupatia eneo hili ekari 10 lakini tumepewa mlima mwingine ekari hazipungui 70 za matumizi ya halmashauri na hakuna fidia yeyote"alisema Valentino Hongoli

Naye Edwin Swale alisema "Tumejipanga kuendelea na miradi ya serikali katika jimbo hili"

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo Akiwemo Roida Wandelage,Neema Mbanga na Paulo Kinyamagoha Wamepongeza Maamuzi ya Serikali  Kuridhia Maamuzi Yao Huku Wakitaka Kuendelea Kushughulikiwa Kwa Changamoto Mbalimbali zikiwemo za Miundombinu ya Barabara Pamoja na Tatizo la Wakulima wa Chai Kucheleweshewa Malipo yao.

Tangu Mwaka 2019 Serikali Ilipotangaza Kila Halmashauri Kuhamia Katika Maeneo Yao ya Kiutawala Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ilikuwa Ikitolea Huduma Katika Kijiji Cha Lunguya Kwa Muda Hadi Sasa Serikali inapobariki Maamuzi ya  Madiwani Juu ya Eneo la Ujenzi wa Makao Makuu.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe, Ummy Mwalimu (MB)  akilizia ujenzi wa makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Njombe na kuagiza ujenzi uanze mara moja hapo kesho.

B:Baadhi ya watumishi na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe pamoja na watumishi wa mkoa wa Njombe wakisikiliza maelekezo ya waziri Ummy alipokuwa ameketi na watumishi hao katika ukumbi wa shule ya sekondari Mtwango uliopo kata ya Mtwango ili kuzungumzia changamoto mbali mbali za halmashauri hiyo pamoja eneo la ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo.



 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini