Mtangazaji maarufu na kipenzi cha wengi nchini @millardayo ameshea mengi na watanzania namna Clouds ilivyomlea na mchango wa mkurugenzi wa media hiyo @josephkusaga kwenye ukuaji wa Millardayo.com
Millard amedai kufanya kazi chini ya Joseph Kusaga kuna utofauti mkubwa na sehemu alizowahi kupita na si kwa lengo la kudharau alipopita,kwanza kabisa kupewa uhuru wa kuipromote media yake ndani ya media ya Clouds na kuzidi kutafutiwa connection za Millardayo.com na Joseph kusaga bila kusaga kufaidika na chochote kile na blog hiyo.
Lakini pia Millard amemshukuru mkuu wa wilaya ya Kinondoni,mh @ggondwe kwa Imani yake kwake,kumuamini tokea wakati huo na kumpa malipo ya sh. Laki 3 kwa tangazo ambalo Millard aliwahi kulifanya mwaka 2006 fedha ambayo hakuwahi kuiwaza kwa wakati huo.
Gondwe ni moja ya watu waliohudhuria Mchongo wa Big Jo hii leo
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments