WAZIRI KABUDI: WATUMISHI WAZEMBE, WAPENDA RUSHWA HATUTA WAVUMILIA | ZamotoHabari.


 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge (kushoto) akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi  alipowasili mkoani hapa kwa ziara yake ya kikazi juzi ambapo tayari ametembelea wilaya ya Singida, Mkalama na Iramba. 


Na Dotto Mwaibale, Singida

WAZIRI  wa Katiba na Sheria Profesa  Palamagamba Kabudi amewaagiza Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma katika utendaji wao wa kazi wa kila siku hasa katika utoaji wa haki kwa wananchi. 

Kabudi ametoa kauli hiyo kwa Nyakati tofauti wakati akizungumza na Watumishi wa Mahakama na Wadau wa Sheria katika wilaya za Singida na Halmashauri ya Mkalama na kusisitiza kuwa wizara yake haitawavumilia watumishi wazembe na wapenda rushwa kwani wakiachwa bila kuwajibishwa wataipata matope Idara ya Mahakama.

Wizara yangu haitawavumilia watumishi wazembe na wapenda rushwa kwani wakiachwa bila kuwajibishwa wataipata matope Idara ya Mahakama ili ionekane kuwa haifanyi kazi zake vizuri kumbe hali hiyo inasababishwa na watumishi wachache," alisema Profesa Kabudi.

Akizungumzia kuhusu uhaba wa Watumishi wa Mahakama Kabudi alisema Serikali itahakikisha inaondoa changamoto hiyo haraka ili wananchi waweze kupata huduma bora na ya uhakika karibu na maeneo yao.

Aidha alisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyika kazi kwa Watumishi wa Mahakama ikiwemo kupatia vitendea kazi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.



APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini