Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jijini, kikosi cha KMC FC hapo kesho kitaanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa siku ya Jumamosi ya Februali 26 mwaka huu.
KMC FC jana ili ibuka na ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Dodoma Jiji na kwamba kikosi hicho leo kitapumzika na kesho kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa pili ambapo matokeo ya mchezo wa jana yanatoa nafasi kwa Timu kuendelea kujipanga vizuri kwenye mchezo unaokuja.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thiery Hitimana imejipanga kufanya vizuri kwenye michezo ya mzunguko wa pili ili kuzidi kujiimarisha katika nafasi ya msimamo wa Ligi kuu na hivyo kumaliza ligi kwenye nafasi ambayo klabu ilijiwekea malengo ambayo ni nafasi tatu za juu.
“Tumepata matokeo mazuri ambayo tuliyahitaji kwa namna yake katika mchezo huo, ulikuwa mchezo mgumu lakini ubora wa wachezaji tulionao ndio uliamua matokeo ya mchezo wetu wa jana, hivyo tunawapongeza kwa kazi kubwa ambayo waliifanya ya kuleta furaha kwa mashabiki zetu ambao kila siku wamekuwa mstari wa mbele kuisapoti Timu.
“ Kitu kikubwa ambacho tulikifanya ni kutumia nafasi vizuri ambazo tulizipata, wachezajii na Benchi la ufundi lilijipanga vema kwenye mchezo huo kwasababu tulifahamu tunakutana na timu ambayo imetoka kupoteza hivyo nilazima kucheza kwa tahadhari na umakini mkubwa, tunamshukuru Mungu tulifanikiwa na kuondoka na alama tatu muhimu na magoli mawili ambayo yalifungwa na Awesu Awesu pamoja na Hassan Kabunda.
Kwenye msimamo wa Ligi kuu kwasasa tupo nafasi ya tisa ambayo bado sio nafasi nzuri kwetu, hivyo kikubwa tutazidi kutumika kwa hali na mali ili tuendelee kupanda kwenye nafasi nzuri zaidi ambayo klabu iliweka malengo yake na hilo ni jambo ambalo linawezekana kabisa kwa sababu michezo yote ipo ndani ya uwezo wetu.
Hadi sasa KMC FC imecheza michezo 15 ikiwa kwenye nafasi ya tisa (9) katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara ambapo kati ya michezo hiyo imeshinda mechi Nne, sare 7 na kupoteza michezo mitatu hivyo kwasasa Timu inaelekeza nguvu kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ambao ni dhidi ya Polisi Tanzania ili kufanya vizuri zaidi.
Imeandaliwa leo Februali 21
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments