MANARA APEWA SHAVU BODABODA MKOMBOZI KWA WATANZANIA. | ZamotoHabari

Ahaidia kutoa Elimu ya usalama Kwa Madereva wa pikipiki

  Na.Khadija Seif, Michuzi TV

WATU Wenye ushawihi katika jamii washauriwa kuheshimu na kujenga nidhamu ya Hali ya pindi wanapoteuliwa kuwa Mabalozi katika Makampuni.

Akizungumza hayo Balozi wa Kampuni ya Sunbeam yenye chapa ya pikipiki ya Hero febuari 21, Haji Manara amesema mara nyingi Kampuni zimekuwa zikitoa fursa za watu wenye ushawihi kwenye jamii kuzitangaza Kampuni hizo hivyo waonyeshe juhudi na kuwaaminisha kuwa wamefanya uchaguzi sahihi katika uteuzi huo.

Haji Manara mapema Leo, ameteuliwa kuwa Balozi wa Kampuni hiyo na kuibeba rasmi Kampeni ya "Piga gia Barabara ishangae".

Pia ahaidia kufanya kazi Kwa ushirikiano mkubwa na Kampuni hiyo Huku akisisitiza swala la kutoa Elimu Kwa madereva wa pikipiki kutumia "kofia" Kwa usalama wao na abiria Ili kupunguza Kasi ya ajali za Barabara.

Aidha,Meneja Masoko wa Kampuni hiyo ambayo mpaka Sasa imeshasambaza takribani pikipiki milioni 1 duniani,Nadah Dhiyebi amesema Kampuni ya Hero Motorcorp inaongoza Kwa kutengeneza na kuzalisha pikipiki zinazoongoza Kwa ubora duniani.

"Pikipiki zinapatikana nchi nzima Kwa Mawakala wajiosajiliwa ambapo mpaka Sasa wapo Mawakala 27 wapo Kwa ajili ya kukuhudumia."

Hata hivyo Dhiyebi ameeleza kuwa bidhaa hizo zimekuja kuwakomboa watanzania Kwa kuingiza nchini pikipiki za Hunter ambazo ni hunter 100 na kuhaidi kushirikiana na Balozi huyo mpya.

Balozi mpya wa Kampuni ya Sunbeam wa chapa yake ya "Hunter" akitambulisha pikipiki aina ya "chombo ya Mishe" mara baada ya kutambulisha rasmi kuwa Balozi na kuhaidi kushirikiana nao katika kuhakikisha wateja wanapata vitu vizuri Kwa Mazingira halisi

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini