Kikosi cha KMC FC hapo kesho kitashuka katika Dimba la Azam Complex Chamanzi Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa saa 1:00 jioni.
Mchezo huo wa kufunga mzunguko wa kwanza utapigwa ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kupisha michuano ya Kombe la Azam Sport Federation kwa mujibu wa ratiba ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha mkuu Thierry Hitimana imefanya maandalizi yake ya mwisho na kwamba ipo tayari kwa mtanange huo na hivyo kuhakikisha kwamba inaondoka na alama tatu muhimu.
KMC FC itaingia kwenye mchezo wa kesho ikihitaji ushindi muhimu licha ya kwamba utakuwa na ushindani mkubwa lakini maandalizi yaliyofanyika yatakuwa na matokeo makubwa kwenye mchezo huo.
“Tunakwenda kwenye mchezo ambao ni muhimu kwa kila Timu, KMC tunahitaji ushindi lakini pia wenzetu wa Dodoma Jiji nao pia wanahitaji ushindi, hivyo ushindani utakuwamkubwa sana tena mkubwa lakini hautazuia Manispaa ya Kinondoni isipate alama tatu muhimu.
Tumefanya maandalizi ya kutosha, hakuna kitu ambacho kitazuia Timu Bora KMC FC kupata ushindi, wachezaji wanamorali kubwa sana, na siku zote wachezaji wamekuwa wakipambana kwa ajili ya kupata matokeo, hivyo mashabiki waje uwanjani kusapoti Timu sambamba na kushuhudia burudani nzuri ya soka.
Kwaupande wa hali za wachezaji wote wako vizuri na kwamba hakuna mchezaji yeyote ambaye anaweza kukosekana kwenye mchezo huo kwasababu mbalimbali hivyo suala la nani ataanza kwenye mtanange huo hilo ni jukumu la kocha kadiri ambavyo atahitaji.
Imetolewa leo Februali 19
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments