SIMON ATAMBA KUTANGAZA LUGHA YA KISWAHILI KWA MUZIKI | ZamotoHabari



MKALI anayetangaza Lugha ya Kiswahili kupitia muziki wa kizazi kipya anayeishi  nchini Australia, Simon Masanja, maarufu kama Simorix The General ‘Jenerali’, ametamba kunogesha mwezi wa wapendanao (Valentine Day) na wimbo wake mpya Vaccine.

Mkali huyo aliyewai kutamba na ngoma kama Tunapiga bao Simorix the General amesema kwa msimu huu watu waburudike na ngoma kali inayokwenda Kwa jina la Vaccine.

Akizungumza kwa njia ya simu mapema leo Simorix, amesema  kuwa wimbo huo wa Vaccine au Chanjo imepokelewa vizuri kwasababu ya ujumbe mzuri wa mapenzi kwenye msimu huu wa wapendanao.

“Vaccine imeanza kufanya vizuri hapa Australia katika kipindi hiki cha Valentine, ninaongelea penzi kama chanjo, naamini kila mtu ana mpenzi wake ambaye ana umuhimu mkubwa kwenye maisha yake na huu wimbo ni maalumu kwaajili yao,” amesema Simorix.

“Msimu wa Valentine una mambo mengi sana wapenzi wanagombana na wapo ambao Ndio wanaanzisha mahusiano hivyo nikaona na Mimi nitoe zawadi hii Kwa mashabiki zangu wote hasa wanaopenda mziki mzuri”

“Kiukweli sikutegemea kama ngoma yangu ya “VACCINE” itapokelewa vizuri kiasi hiki na nimeiachia siku special ambayo ni siku yangu ya kuzaliwa. Imepokelewa vizuri sana hapa Australia natarajia itafanya vizuri Tanzania pia”mesema General.

“Kiu yangu kubwa ni kupeperusha bendera ya Tanzania nchini Australia kupitia bongo flavour nipende kuwa ambia mashabiki zangu watembelee channel yangu ya youtube ambayo ni -SIMORIX THE GENERAL” amesema General.

Simorix The General mpaka sasa anatamba na kibao chake cha ‘tuna piga bao’  wimbo ukiwa imetengenezwa na Kimambo na Director wa video ni Daniele Cernera kutokea Australia pamoja na hit song mpya kwa sasa VACCINE


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini