SIMBA SC KUFA AU KUPONA NYUMBANI BENJAMIN MKAPA | ZamotoHabari

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Simba SC italazimika kupata ushindi katika mchezo wake wa mwisho na wa muhimu wa Kundi D la Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya US Gendermarie Nationale ya Niger, ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele ya Michuano hiyo, kwenye mchezo huo utachezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Katika mchezo wake dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, Simba SC imepoteza kwa mabao 3-0 kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Stade de l'Amitie nchini Benin. Asec Mimosas walipata mabao yao kupitia kwa Kramo Kouamé dakika ya 16, Stephen Azizi KI dakika ya 25 na Karim Konaté dakika ya 57.

Simba SC watalazimika kupata ushindi katika mchezo wa mwisho wa Kundi hilo dhidi ya USGN hiyo na endapo watapata sare, itategemeana na matokeo ya RS Berkane ya Morocco ambao wao wamepata sare ya bao 2-2 dhidi ya wenyeji USGN dakika za mwisho, katika mchezo uliochezwa muda mmoja baina ya Simba SC na Asec.

Msimamo wa Kundi D, Asec Mimosas wanaongoza wakiwa na alama 9 wakati, RS Berkane na Simba SC wakifungana alama wote wakiwa na alama 7 huku USGN wakibura mkia wakiwa na alama 5 pekee.

Raundi ya mwisho, Simba SC watakuwa nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa wakiikaribisha USGN, Aprili mosi, 2022 wakati RS Berkane watawakaribisha Asec Mimosas mjini Berkane nchini Morocco. Matokeo ya ushindi kwa Simba SC yataipeleka katika Robo Fainali ya Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.





Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini