Waziri Mchengerwa awataka watendaji kuchapa kazi | ZamotoHabari


Na. John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka Watendaji wote wa Wizara yake kujitafakari utendaji wao na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuendelea kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya wakati alipokuwa akifungua kikao cha kupitishwa kuhusu maandalizi ya Bajeti na Randama kwa mwaka wa fedha 2022/23 na kamati ya bajeti leo Machi 20, 2022 katika ukumbi wa MAELEZO jijini Dodoma.

"Naomba niwatake watendaji wote kufanya kazi kwa kufuata maadili na taratibu za kazi za Serikali ili kuleta
mafanikio kwa wananchi kwa ujumla". Amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha, amewataka Wakuu wa Idara wote kuwa na vikao vya kiutendaji na watumishi wao ili kuleta mageuzi ya kiutendaji.

Pia amewataka watendaji kufanya kazi kama timu mmoja huku wakifungua milango ya wadau kama wasanii ili kujua haki zao.

“Watendaji tokeni waelezeni wasanii ili waweze kujisajili ili waweze kupata haki zao na wapate manufaa”. Amesisitiza Mhe. Mchengerwa

Kwa upande mwingine, Mhe. Mchengerwa amesema Wizara imefanya mambo makubwa kwenye sekta za michezo, sanaa na Utamaduni na kwamba kinachotakiwa sasa ni kuendelea kufanya vizuri.

Aidha, ametumia tukio hilo kumshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kusaidia sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali yake.




 
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini