WATANO WALIA, WATANO WACHEKA KUFUZU KOMBE LA DUNIA, UKANDA YA AFRIKA | ZamotoHabari


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

NDIO! Watano wamecheka na Watano wengine wamelia, katika kuwania nafasi ya Kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Kanda ya Afrika, katika michezo iliyochezwa nyumbani na ugenini, kati ya Machi 25 na 29, 2022 katika bara hilo la Afrika.

Waliocheka baada ya kufanikisha azma yao ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka huu wa 2022 kati ya timu 10, ni timu za taifa za Cameroon, Tunisia, Morocco, Senegal na Ghana ambao watawakilisha Kanda ya Afrika katika Michuano ijayo ya Kombe la Dunia na timu zilizolia baada ya kushindwa kufuzu Michuano hiyo ni Algeria, Misri, Mali, Nigeria na DR Congo.

Hatua hiyo ya tatu ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika, mchezo ambao uliwavutia wengi ni ule, kati ya Senegal dhidi ya Misri mchezo uliohitimishwa kwa mikwaju ya Penalti na Senegal kufuzu Michuano hiyo mikubwa duniani kwa Penalti 3-1 dhidi ya Misri.

Mchezo huo ulikuwa kumbukumbu ya Fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) yaliyofanyika nchini Cameroon kwa Simba wa Teranga, Senegal kuibuka Mabingwa baada ya kuwafunga Misri kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti.

Hata hivyo, safari hii walikutana mara mbili, yaani nyumbani na ugenini, mchezo wa kwanza, Senegal walikubali kichapo cha bao 1-0 katika dimba la Kimataifa la Cairo, nchini Misri wakati mchezo wa marudiano mjini Dakar wenyeji Senegal waliibuka na ushindi wa bao 1-0 hivyo kupelekea kuongezwa dakika 30 na kufanya kutimia dakika 120 za mchezo huo.

Mchezo mwingine, ulikuwa kati ya Cameroon dhidi ya Algeria, mchezo ulioisha kwa matokeo ya kikatili kwa Cameroon kufuzu Kombe la Dunia 2022 katika ardhi ya ugenini, kwa faida ya bao la ugenini la dakika za mwisho. Cameroon wakiwa chini ya Kocha wao Rigobert Song wamefunzu Kombe la Dunia kwa matokeo ya bao 2-2 licha ya kufungwa bao 1-0 nyumbani kwao mjini Douala na kupata ushindi wa bao 2-1 mjini Blida katika uwanja wa Mustapha Tchaker, Algeria.

Timu ya taifa ya Morocco, imefuzu Michuano ya Kombe la Dunia 2022 baada ya kuishushia kichapo timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mabao 4-1 katika dimba la Mohammed V mjini Casablanca na kufanya jumla ya mabao 5-2 baada ya sare ya awali ya 1-1 katika mji wa Kinshasa nchini DR Congo, Uwanja wa Pentecost Martyrs.

Ghana wamefuzu Kombe la Dunia 2022 kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kupata sare ya 0-0 nyumbani kwao katika mji wa Kumasi kwenye dimba la Baba Yara. Katika mchezo wa mkondo wa kwanza, The Black Stars wamefuzu Kombe la Dunia baada ya kuilazimisha sare ya bao 1-1 timu ya taifa ya Nigeria katika mji wa Abuja.
Morocco wamefuzu Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi wa jumla wa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliopigwa Machi 25, 2022 nchini Mali. Tunisia walilazimishwa sare ya 0-0 katika mchezo wa mkondo wa pili uliochezwa nchini Tunisia katika dimba la olympique de rades.



 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini