Picha ya Pamoja.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa , Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) amesema kuwa anayo mengi ya kujivunia kwa timu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Golf ya Wanawake (TPDF Lugalo Golf Club) yakiwemo ya kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi. Timu hii imeenndelea kufanya vizuri kwa kuibuka washindi inapocheza na timu za ndani na hata zile za nje ya nchi.
“Yapo mengi ya kujivunia katika klabu hii, hasa Timu ya Gofu ya wanawake. Kweli Timu hii inaitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi na hasa inapocheza nje ya nchi. Mliweza kushinda mlipoenda kucheza Nigeria, mliweza kushinda mlipoenda kucheza Ghana, mliweza kushinda mlipoenda kucheza Kenya, na mliweza kushinda mlipoenda kucheza Uganda. Na mmeweza kutoa mchango mkubwa kwa Timu ya Taifa”, alisema.
Mheshimiwa Tax ameyasema hayo wakati akiwa Mgeni Rasmi wakati wa kufunga Mashindano ya Lugalo Ladies Open 22 yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 21 – 22 Mei, 2022 katika Viwanja TPDF Lugalo Golf Club, mashindano yaliyozishirikisha Timu sita, Timu mbili kutoka kila mkoa kwa mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na kilimanjaro.
Akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuongea na wageni waalikwa, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema kuwa mashindano haya yamepangwa na kuratibiwa na wanawake wenyewe. “Kiukweli hadi kufanikiwa kwa mashindano haya wanawake wenyewe wameanzisha, wamejipanga hadi kusimamia mashindano haya”, alisema.
Dkt Stergomena amewapongeza washiriki wa mashindano hayo kwa ushiriki wao na kwa namna walivyohamsika na kuamua kushiriki kwa wingi licha ya majukumu mengi yanayowakabili. Vile vile ameupongeza uongozi wa TPDF Lugalo Golf Club kwa jitihada zake za kuiunga mkono pamoja na kuibua vipaji kwa wanawake.
Pia, Mheshimiwa Waziri amewapongeza washiriki walioibuka washindi na kutunukiwa zawadi mbalimbali zikiwemo vikombe, tiketi za ndege na Fridge. Kwa kuwa michezo ni burudani, amewasihi wale wote ambao hawakufikia ushindi wasikate tama bali waendelee kushiriki. Aidha, amewashukuru wadhamini kwa kuona umuhimu wa kudhamini na hatimaye kufanikisha mashindano hayo.
Mbali na kufunga mashindano hayo Mheshimiwa Waziri aliongoza Harambee ya kuchangia Mfuko wa Wanawake wa Wacheza Gofu ambapo yeye binafsi aliweza kuchangia shilingi milioni 25 taslimu ili kuiwezesha timu hiyo kushiriki mashindano yatakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu nchini Kenya.. Aidha, ameahidi kuendelea kuisaidia timu hiyo kwa kadri atakavyoona inafaa. Pia, amezitaka timu za wanaume nazo zijitahidi kufanya vizuri ili kuitia moyo timu ya wanawake wachezag gofu.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na makampuni mbalimbali na watu binafsi yakiwemo QatarAir, Akiba Commercial Bank, PrecionAir, GreatLakes, sana, SBC (Pepsi), Angels, Serena Hotels, Mohammed Enterprises Limited, Johnie Walker na 24/7 Adventure.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments