Mkurugenzi Mkuu wa Manjano Foundation, Shekha Nasser katikati akizungumza leo Mei 23, 2022 jijini Dar es Salaam, wakati wa kuwakaribisha Manjano Dream Makers 30 kwaajili ya mafunzo ya wiki mbili yanayoanza leo Mei 23, 2022 hadj Juni 3, 2022.kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo Chuo cha Manjano Foundation, Alai Haleed na kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo idara ya usimamizi wa mapambo taasisi ya Manjano Foundation, Rose Kimaro
Mkurugenzi Mkuu wa Manjano Foundation, Shekha Nasser akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wanawake na wasichana, Manjano Dream Makers 30 kwaajili ya mafunzo ya wiki mbili kuanzia Leo Mei 23, 2022 hadj Juni 3, 2022.
Mkurugenzi wa Mafunzo Chuo cha Manjano Foundation, Alai Haleed akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mei 23, 2022 wakati wa kuwakaribisha Manjano Dream Makers 30 kwaajili ya mafunzo ya wiki mbili kuanzia Leo Mei 23, 2022 hadj Juni 3, 2022. kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Manjano Foundation, Shekha Nasser
Mkurugenzi wa Mafunzo idara ya usimamizi wa mapambo taasisi ya Manjano Foundation, Rose Kimaro akizungumza leo Mei 23, 2022wakati wa kuwakaribisha Manjano Dream Makers 30 kwaajili ya mafunzo ya wiki mbili kuanzia Leo Mei 23, 2022 hadj Juni 3, 2022.
Wasichana na wanawake wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Manjano Foundation, Shekha Nasser wakati akizungumza na kuwakaribisha Manjano Dream Makers 30 kwaajili ya mafunzo ya wiki mbili yanayoanza leo Mei 23, 2022 hadj Juni 3, 2022.
Baadhi ya wasichana na wanawake Manjano Dream Makers 30 wakipewa maelekezo na Mkurugenzi Mkuu wa Manjano Foundation, Shekha Nasser mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Manjano beauty jijini Dar Es Salaam leo Mei, 23, 2022 kwaajili ya kuanza mafunzo ya wiki mbili.
Picha ya Pamoja.
KATIKA kusherehekea miaka Saba (7) tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya MANJANO FOUNDATION imeanza kutoa mafunzo kwa Manjano Dream-Makers 30 kuanzia leo Mei 23, 2022 mpaka Juni 3, 2022.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha Manjano Dream Makers 30, leo Mei 23, 2022 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser amesema Jumla ya wasichana na wanawake 30 watapata mafunzo hayo kwa muda wa wiki mbili (bure) bila malipo yeyote na Mafunzo hayo yatatolewa katika fani ya ujuzi na ubunifu katika tasnia ya vipodozi yaani 'Make-up Artist' na 'event planning' yaani kupamba ukumbi.
"Tasnia ya Urembo ni kama Tasnia nyingine yeyote ile nyingine, hata wachezaji mpira, unamwona Ronald kocha wake anamfundisha. Lakini Kocha anaweza kuwa kama Ronald? Na tasnia ya urembo ipo hivyo hivyo, kwahiyo mimi nakufundisha lakini wewe unatakiwa kuwa 'best Vizuri zaidi, unatakiwa 'ushine'." Amesema Shekha
Amewaasa Manjano Dream Makers 30 kuwa na Juhidi wakati wa kujifunza ili wawe bora zaidi.
Licha ya hayo Shekha akiwaonesha maeneo ya kujifunzi pia amewaelekeza jinsi mafunzo hayo yatavyotolewa ndani ya wiki mbili.
Licha ya hayo Shekha amewakaribisha kujiunga na mafunzo ya ngozi kwani mafunzo hayo yanachukua muda wa miaka mitatu ili kuifahamu zaidi ngozi ya binadamu.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa mafunzo na Idara ya Usimamizi wa Mapambo, Rose Kimaro amesema kuwa ndani ya wiki hizo mbili Manjano Dream Makers 30 watajifunza namna ya Kupamba katika harusi, kupamba kumbi za kumbukumbu za kuzaliwa, kupamba kumbi za 'Bridle shower' pamoja na kupamba Sherehe za kiserikali.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Mafunzo, Chuo cha Manjano Beauty Academy, Alai Haleed amewaasa 'Manjano Dream Makers 30' kutumia mafunzo yanayotokea mara chache kwa mwaka pia amewapongeza wale wanaochangamkia fursa pale zinapojitokeza.
Pia amesema kuwa wanapima na kurudisha mchango kwa jamiii baada ya kufundisha kwa muda Mrefu.
Pia amewahamasisha wale ambao hawajafanikiwa katika kipindi hiki wawe karibu ili kujipatia fursa hiyo ambayo hutolewa mara chache katika kipindi kirefu
"Urembo unalipa unalipa." Haleed alimalizia kusema.
Taasisi ya MANJANO FOUNDATION imekuwa ikitoa mafunzo hayo bure tangu Mei 2015 kwa Manjano Dream-Makers 30 ikiwa program hiyo ni ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia Kipodozi cha LuvTouch Manjano.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments