GEITA GOLD FC WAKOSA TSH. MIL 30/- ZA MKURUGENZI | ZamotoHabari


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

KIKOSI cha Geita Gold FC kimekosa kiasi cha fedha Shilingi Milioni 30/- baada ya kupata sare ya bao 1-1 na Kikosi cha Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Mji wa Geita, Mhe. Zahara Michuzi aliahidi kiasi hicho cha fedha endapo Kikosi cha Matajiri wa Dhahabu kikipata ushindi mbele ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Geita Gold FC walianza kupata bao katika dakika ya 19 kupitia kwa Mshambuliaji wake kinara, George Enock Mpole baada ya Walinzi wa Simba SC kushindwa kuondoa mpira uliokuwa una zagaazagaa katika lango lao.

Dakika ya 25, Simba SC walisawazisha bao hilo kupitia kwa Mshambuliaji wao, Kibu Dennis Prosper baada kupiga Kichwa safi kilichowashinda Golikipa na Walinzi wa Geita FC na kujaa wavumi.

Baada ya mchezo huo, Geita Gold FC wanafika alama 35 na michezo yao 25 watabaki kwenye nafasi ya 5 ya msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, wakati Simba SC wakibaki kwenye nafasi ya pili na alama zao 51 na michezo 25.



 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini