Na Mwandishi Wetu
KWAYA maarufu nchini ya Gethsemane Group Kinondoni (GGK) SDA wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam wametoa video mpya ya wimbo ujulikanao kwa jina la 'Bado Kitambo'.
Kwaya hiyo imejizolea umaarufu kutokana na mstari wa mbele kufariji taifa hususani pale walipotunga wimbo maalumu baada ya ajali ya meli ya MV. Nyerere na hata taifa lilipo ondokewa na aliyekua Raisi wa awamu ya tano Dk. John Magufuli, Gethsemane walikua moja ya kikundi cha uimbaji cha mwanzo kabisa ambao walitoa wimbo wa Faraja Kwa taifa. Wimbo ambao ulipokelewa vizuri Kwenye Jamii pamoja na vyombo Vya Habari.
Kwa mujibu wa uongozi wa kundi hilo umesema leo jijini Dar es Salaam kuwa baada ya kutoa video mbalimbali na kupokelewa vyema, kwa sasa wametoa video mpya ya wimbo uliopewa jina la 'Bado Kitambo' ambao ni mahususi katika kuwakumbusha wanadamu kuwa Duniani tunapita.
"Ila pamoja na changamoto zote za dunia, ipo ahadi kwamba kuna Tumaini jipya Kwa wale washindi wa dhambi. Tuna imani kwamba wimbo huu utandelea kubariki watu wa imani na dini zote na kuendelea kumtumaini Mungu na kushinda dhambi”,alisema mmoja wa Viongozi wa Kwaya hiyo.
Uongozi wa Gethsemane umefafanua zaidi kwamba wimbo huo utakuwepo kwenye album yao mpya inayotarajiwa kutoka mwaka huu. “Tumeona wakati tunaendelea kurekodi album ambayo itakua na Nyimbo kumi, basi tuwape mashabiki wetu kionjo kidogo waendelee kubarikiwa wakati sisi bado tukiendelea na kurekodi. Tuna imani album Hii itakua baraka Kwenye Jamii. Wimbo wa bado kitambo unapatikana Kwenye Chanel yetu ya YouTube.”
Wana kwaya wa Gethsemane wakiimba wa wimbo unaofahamika Bado Kitambo ambao video yake tayari iko kwenye YouTube
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments