Na.Khadija Seif, Michuzi TV
WAJASIRIAMALI watakiwa kushiriki katika fursa za Mashindano yanayojitokeza Ili kuendelea kuwajengea uwezo na morali ya kuwajibika katika fani na biashara zao.
Akizungumza na Michuzi, Balozi wa maonyesho ya Tuzo za Zikomo, Kulwa Mkwandule'son ambae ni Mbunifu wa Mavazi Kwa miaka 8 nchini Tanzania amesema kuwepo Kwa tuzo hizo akiwa kama mshiriki wa Msimu wa pili kumeweza kumpa mwangaza na kuboresheka Kwa harakati zake za Ubunifu Kwa kuona jinsi gani kazi anazozifanya zinakubalika katika jamii yake na nje ya nchi.
"Kabla sijatambua umuhimu wa designers naomba niwashukuru wazazi wangu Baba Yangu Mr Mkwandule apumzike kwa Amani pia mama yangu kipenzi ambae amekuwa akinisukuma kufanya haya ninayofanya leo Maria Mdaki nawashukuru pia walezi wangu kwa support yao Mr.& Mrs Hamis Matanda,Mr & Mrs Mayila,Mrs Sophia Mushi na Ms Monica Ramadhan nawashukuru sana hao ni Miongoni mwa watu wanaonitia moyo nakuona fahari Kwa kile ninachokifanya Kila iitwapo Leo na kuthubutu kushiriki Tuzo hizo Kwa mara ya pili."
Aidha ameeleza kuwa Kwa mwaka huu Tuzo hizo zitafanyika Jiji la Lusaka nchini Zambia ikiwakutanisha watu mbalimbali wakiwemo Wasanii, wabunifu,djs Huku akitoa taarifa rasmi kuongezeka Kwa vipengele vingine vya ziada vya tuzo hizo.
"Kwa mwaka Jana kulikua na tuzo takribani 7 lakini Msimu huu ambapo zitafanyika octoba 22 mwaka huu tunatarajia kuwepo Kwa nyiongeza ya Tuzo zisizopungua 10".
Pia ametoa wito Kwa wajasiriamali ambao wangependelea kushiriki waweze kufata vigezo na masharti ya tuzo hizo ikiwemo kujitangaza wao wenyewe kwanza katika Mitandao ya kijamii zaidi Ili kuonyesha uwezo wao .
"Mitandao ya kijamii Ina faida sana Kwa wabunifu kutokana na kutangazika Kwa bunifu zao hivyo napenda kuwashauri kuliko kupoteza muda kuchapisha vitu visivyo na manufaa ni Bora kuweka bunifu zao zaidi katika Kipindi cha zoezi la dirisha la usahili utakapowadia ambapo itakua mapema Juni 2 mwaka huu."
Hata hivyo Mkwandule'son ni Miongoni mwa wabunifu wanafanya vizuri na ambae ameshavalisha watu mbalimbali akiwemo aliekua Waziri wa Sanaa, Michezo na Utamaduni dkt.Harrison Mwakyembe pamoja na watu mashuhuli silaha yake kubwa Mbunifu huyo ikiwa ni kufata yale anayoelekezwa na wabunifu wakongwe akiwemo Jamila vera swai akimtaja kama Mwalimu wake katika sekta ya Ubunifu.
vazi ambalo Mbunifu ambae pia ni Balozi wa maonyesho ya tuzo za zikomo Kulwa Mkwandule'son aliweza kubuni katika Msimu uliopita na akijinasibu Kwa mwaka huu atafanya vitu tofauti zaidi kutokana na tuzo ya mwaka Jana kumpa motisha ya kuwa na weledi zaidi katika bunifu zake.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments