Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
SHIRIKISHO la Kandanda barani Afrika (CAF) limetoa adhabu ya kulipa faini ya Dola 10,000 (zaidi ya Tsh. Mil 20) kwa Klabu ya Simba baada ya kuonyesha vitendo vilivyoashiria imani za kishirikina katikati ya uwanja kabla ya pambano lao la mkondo wa pili dhidi ya wenyeji Orlando Pirates FC kwenye dimba la Orlando mjini Soweto nchini Afrika Kusini.
Barua iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) baada ya maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya CAF, imeeleza kuwa Simba SC wanapaswa kulipa faini hiyo ndani ya miezi miwili (siku 60).
Taarifa ya CAF imeeleza kuwa Wajumbe watatu wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Raymond Hack kutoka Afrika Kusini sanjari na Wajumbe wengine watatu wa CAF walikaa May 8, 2022 na kuthibitisha uwepo wa vitendo hivyo vya Simba SC kuwasha moto katikati ya uwanja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
“Orlando Pirates FC walileta malalamiko CAF kwa vitendo hivyo vilivyoonyeshwa na Simba SC na kusababisha uharibifu sehemu ya katikati ya uwanja, pia Maofisa wetu walikuwepo uwanjani na tumeshuhudia baadhi ya picha na vipande vya video kuhusu tukio hilo”, taarifa imeeleza.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments