Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Waogeleaji wa familia moja Leyna Borega (8) na Lorita Borega (10) wameibuka katika nafasi ya kwanza katika mashindano ya FK Blue Marlins na kushinda vikombe.
Wakati Leyna akishinda kikombe kwa waogeleaji wenye miaka nane na kushuka chini, Lorita alishinda kikombe kwa waogeleaji wenye miaka tisa na 10 katika mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya waogeleaji 233 kutoka klabu 15 za Tanzania Bara na Zanzibar.
Leyna alifanikiwa kushinda medal inane (8) ambapo medali mbili (2) ni dhahabu, tano (5) za fedha na moja ya shaba. Pia mugoeleaji huyo mwenye kipaji alizawadiwa kikombe cha ushindi wa kwanza.
Kwa upande wake, Lorita mbali ya kuwa mshindi wa jumla na kuzawadiwa kikombe, alishinda medali sita (6), ambapo nne (4) za dhahabu na mbili (2) za fedha.
Akizungumza baada ya mashindano hayo, Lorita alisema kuwa siri ya mafanikio yao ni kufanya mazoezi zaidi na kuzingatia mafundisho kutoka kwa walimu wao.
Alisema kuwa wamekuwa wakifanya mazoezi chini ya walimu bora wa klabu ya FK Blue Marlins na vile vile mwalimu wa shule yao ya kimataifa ya Dar es Salaam Independent School (DIS) Haleluya Mpango. Leyna anasoma darasa la nne katika shule hiyo na Lorita anasoma darasa la tano.
“Mashindano yalikuwa magumu sana na kila muogeleaji alikuwa anataka kushinda kama ilivyokuwa kwetu. Tunawashukuru waogeleaji wa klabu ya FK Blue Marlins ma makocha wetu kwa kutupa hamasa na mafunzo na vile vile walimu bora wa shule yao ya kimataifa Dar es Salaam Independent School kwa mafunzo mazuri, mbali ya darasani, pia katika michezo na kutuwezesha kufanya vyema,” alisema Lorita.
Alisema kuwa matokeo hayo yamewapa hamasa kubwa ya kufanya vyema zaidi katika mashindano yajayo na vile vile katika timu ya Taifa ya Tanzania.
Waogeleaji wengine walioibuka washindi katika makundi ya miaka yao ni Ariel Sykes wa klabu ya Champion Rise ambaye alishinda kwa waogeleaji wenye miaka chini ya nane kwa wanaume, Maxi Missokia (9-10, Dar Swim Club), Raya Angemi (miaka 11-12, Taliss-IST), Mulenga Cole (miaka 11-12 wanaume, DSC), Isabela Angemi na Sydney Hardeman (miaka 13-14, Taliss –IST) na Romeo Mwaipasi (miaka 13-14 wanaume, Taliss-IST).
Pia wamo Aravind Raghavendran (miaka 15-16, Taliss-IST), Sofia Latiff (miaka zaidi ya 15, Taliss-IST) na muogeleji nyota nchini, Collins Saliboko wa klabu ya DSC aliyeshinda kikombe kwa waogeleaji wenye miaka kuanza 17 na zaidi.
Lorita Borega (wa kwanza kushoto) na Leyna (katikati) wakiwa pamoja na mama yao Sophia Maduhu
Leyna Borega akishindaka katika mashindano ya kuogelea ya FK Blue Marlins
Waogeleaji wa timu ya FK Blue Marlins wakiwa katika picha ya pamoja.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments