TIBA yasisitiza Bima kwa wanamichezo wote | ZamotoHabari

Chama cha Washauri wa huduma za bima nchini (TIBA) kimetoa rai kwa wasimamizi wa michezo nchini kuweka takwa la kisheria kwa wachezaji kuwa na bima ya ajali na afya ili kuchangia kutoa hamasa na maendeleo ya michezo nchini.

Rais wa TIBA, Amir Kiwanda alisema kuwa kwa sasa msisitizo zaidi umewekwa katika timu za mpira wa miguu za Ligi Kuu na kusahau kuwa Tanzania ina michezo mingi ambao inashirikisha wachezaji ambao wap katika hatari kupata ajili michezoni.

Kiwanda alisema kuwa mchezaji mwenye bima anakuwa na  moyo wa kujituma zaidi uwanjani kwani  endepo anapata tatizo  la kuumia, hatokuwa na wasiwasi katika kupata matibabu.

“Hii ni tofauti na mchezaji ambaye hana bima na hasa ukizingatia kuwa kuna matukio kadhaa ya kusikitisha yanayowahusu wachezaji ambao ilifikia kipindi wadau wanachezesha mechi ili kupata fedha za kusaidia matibabu,”alisema Kiwanda.

Alisema kuwa kazi ya TIBA ni kutoa ushauri kwa watoaji huduma ya bima na wamefanikiwa kwani mpaka sasa kuna huduma nyingi za bima zinazotolewa na makampuni hayo.

Alifafanua kuwa huduma hizo ni muhimu kusaidia kuepuka gharama kubwa za matibabu wanapopatwa na matatizo ya kiafya na janga la kuumia kwenye shughuli za michezo.

Alisema kuwa Tanzania ina michezo mingi na wachezaji wamekuwa wakikumbana na ajali mbalimbali katika michezo na kujikuta kuanza kuangaika katika gharama za matibabu.

Alifafanua kuwa ili kuweza kuwa na mshikamano, wameamua kufanya bonanza la michezo na kushirikisha wadau mbalimbali na kuendelea kutoa ushauri  wa shughuli za bima nchini.

“Bonanza hili ni jukwaa la kuwakutanisha wadau wa bima na kucheza huku tukikumbushana umuhimu  wa utoaji  huduma za bima hapa nchini,” alisema.

Bonanza hilo la tatu lilifanyika kwenye viwanja vya  Don Bosco Namanga na kushirikisha timu ambazo ni TIBA, TAN-RE, IFM, Magnet, Assemble, ATI, TIRA, Sanlam, Alliance, bancassurance na Mawakala.

Wachezaji wa netiboli wakishindana




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini