Na Khadija Kalili
WASANII mbalimbali wa Kizazi Kipya leo Juni, 25,2022 wamefanikiwa kusimamisha Wialaya ya Temeke na viunga vya jirani jijini Dar es Salaam kwa kuwakutanisha mashabiki mbalimbali kwenye tamasha la Kimataifa lililofahamika kama 'Zege Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Mwembe Yanga
Tamasha Hilo ambalo lilinogeshwa na wasanii wenye mvuto katika miondoko mbalimbali ikiwemo singeli, bongo fleva na muziki wa dansi ni pamoja na Ney wa Mitegi, MC Kinata, Maua Sama, Snura Mushi na Mwanamuziki mkongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi Josse Mara.
Mbali ya wasanii hao wengine walio amsha hisia pindi walipopanda jukwaani ni pamoja na msanii Stamina.
Huku wasanii wengine waliokonga nyoyo za mashabiki waliofika kwenye tamasha hilo la 'Zege Day' ni pamoja na Dayoo, Micky Singer, Rasco Sambo, Lody Music, Sir Jay, Nedy Music, Kayumba, Mzee wa Bwax na Sholomwamba.
Akizungumza na waandishi wa Habari wakati tamasha hilo likiendelea mmoja wa viongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group (MMG) Sebastian Maganga amelielezea tamasha hilo la Zege Day kwa kusema kuwa ni la Kimataifa na linafanyika duniani kote hivyo wao MMG wameratibu ikiwa ni katika kutambua na kuthamini mchango wa vijana wauza Chips kwa kuwarahisishia wakazi katika maeneo mbalimbali kupata chakula cha haraka.
"Sote tunajua kuwa maisha ya kimjini yanaratiba ndefu na pana na hapo ndipo utamaduni wa Zege ulipoanzia sisi kama Clouds tumejukita katika kutoa ajira kwa vijana ndipo tulipokaa na kukubalia kuja kufanya tamasha hili hapa Mwembe Yanga baada ya wapenda Zege lialia kupiga kura." Amesema Maganga.
Maganga ameongeza kuwa hakuna historia kamili inayoelezea ni wapi ilianzia Chips Zege lakini historia inasema kuwa watanzania wenye asili ya Bara la Asia ndiyo walianza kuuza Chips maeneo ya Ilala Jijini Dar es Salaam na baadaye chakula hicho kikajizolea umaarufu.
Aidha Maganga amewashukuru wadhamini wa tamasha hilo ambao ni kinywaji baridi cha Pepsi, The Kick na wazalishaji wa sausages.
Msanii wa Bongo Muvi na Muziki wa Kizazi kipya, Snura Mushi akitumbuiza katika tamasha la 'Zege Day' lililofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo Juni 25,2022.
Wasanii mbalimbali wa Muziki wa Kizazi kipya, Snura Mushi wakitumbuiza katika tamasha la 'Zege Day' lililofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo Juni 25,2022.Kampuni ya Clouds Media Group (MMG) Sebastian Maganga akinunua sausage wakati wa tamasha la 'Zege Day' lililofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo Juni 25,2022.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika tamasha la 'Zege Day' lililofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo Juni 25,2022.
Mtangazaji wa Clouds Tv, Sakina Lyoka akiwauzia Chips Zege wananchi waliohudhuria tamasha la 'Zege Day' lililofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo Juni 25,2022.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments