Luiza Mbutu "Tunaisuka CHAMUDATA Mpya wasanii wa Dansi nchi nzima waje kujiunga".

Na Muandishi wetu.

Chama Cha Muziki wa Dansi Nchini (CHAMUDATA) kimewataka wasanii wote wa Muziki wa Dansi kujitokeza kuhisajili kwenye chama hicho pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa( BASATA) ili kuwawezesha kutambulika.
Mwenyekiti wa CHAMUDATA Luizer Nyoni(Luiza Mbutu) akiongea na waandishi wa Habari ambao hawapo pichani mapema leo mkoani Dar es salaam.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Luizer Nyoni maarufu Kama mama "Luizer Mbutu"wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kuelezea mwelekeo mpya wa Chama hicho baada ya kupata uongozi mpya 

Amesema kwamba wasanii wengi wa Dansi hawajajisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na CHAMUDATA hivyo kutokana na kupatikana na uongozi mpya wa Chama hicho kinawasihi kuhisajili ili kufikia malengo yao kwani CHAMUDATA ya Sasa imejiwekea malengo makubwa.

"Sisi kama viongozi wapya tuna  vipaumbele kumi tutakavyo vitekeleza ikiwa ni pamoja na kueneza CHAMUDATA nchi nzima, kuandaa semina ya mafunzo ya hakimiliki na hakishiriki na mirahaba ambapo tayari tumezungumza na COSOTA ili watupe mafunzo,pia kukutana na viongozi wa bendi mbalimbali ili kuainisha changamoto zinazowakabili Wanamuziki na Biashara ya Muziki Kwa Ujumla." amesema Luizer

Nakuongeza kuwa vipaumbele vingine ni kushirikiana na vyombo vya habari katika kuutangaza Muziki wa Dansi,kutengeneza tovuti ya CHAMUDATA Ili kusaidia wanachama kuhisajili kidigitali,kusimamia masuala ya Bima ya afya Kwa wanachama,kuiwezesha CHAMUDATA kuwa karibu na serikali ili kutatua changamoto zinazowakabili,kuhakikisha bendi zote zinazofanywa maonyesho zimesajiliwa BASATA pamoja na kuandaa Tamasha kubwa la Muziki wa Dansi.
Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Bw. Said Kibiriti akijibu swali la Muandishi wa habari mapema leo Mkoani Dar es salaam.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHAMUDATA  Bw.Said Kibiriti amesema kwamba uongozi uliopo Kwa sasa ni uongozi mpya,baada ya kukabidhiwa ofisi na uongozi wa zamani baadhi ya nyaraka za ofisi hazipo nakwamba baada takufatilia wamebaini baadhi ya viongozi hao wameshafariki,hivyo kumekuwepo na madeni huku akaunti za chama  za  NMB na CRDB zikiwa hazina fedha.

" Hatuna Hesabu Sahihi ya madeni kwasasa,lakini bado tunaendelea kuyakusanya na yakiwa tayari tutawafahamisha wanachama,kwasasa tuanaendelea kukiimarisha chama kwani kimeanzishwa tangu mwaka 1986 lakini bado kimekuwa hakifahiki vizuri kwa wanamuziki wa Dansi Nchi nzima" amesema Bw.Kibiriti.
Mkutano ukiendelea.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini