UONGOZI MPYA CHAMUDATA YA AINISHA KUKABILIWA NA MADENI YA AWALI | ZamotoHabari

CHAMA cha Muziki wa Dansi Nchini (CHAMUDATA) kimewashauri wasanii wote wa Muziki wa Dansi kujitokeza kujisajili kwenye chama hicho pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa( BASATA) ili kuwawezesha kutambulika.

Akizungumza na waandishi wahabari Mwenyekiti wa chama hicho Luizer Nyoni maarufu kama mama "Luizer Mbutu" na kueleza mwelekeo mpya wa chama hicho baada ya kupata uongozi mpya.

Amesema kwamba wasanii wengi wa dansi hawajajisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pamoja na (CHAMUDATA )hivyo kutokana na kupatikana na uongozi mpya wa chama hicho kinawasihi kujisajili ili kufikia malengo yao kwani CHAMUDATA ya Sasa imejiwekea malengo makubwa.

"Sisi kama viongozi wapya tuna vipaumbele kumi tutakavyo vitekeleza ikiwa ni pamoja na kueneza CHAMUDATA 
nchi nzima,kuandaa semina ya mafunzo ya hakimiliki na hakishiriki na mirahaba ambapo tayari tumezungumza na COSOTA ili watupe mafunzo,pia kukutana na viongozi wa bendi mbalimbali ili kuainisha changamoto zinazowakabili Wanamuziki na Biashara ya Muziki mwa ujumla."

Nakuongeza kuwa vipaumbele vingine ni kushirikiana na vyombo vya habari katika kuutangaza Muziki wa Dansi,kutengeneza tovuti ya CHAMUDATA Ili kusaidia wanachama kuhisajili kidigitali,kusimamia masuala ya Bima ya afya Kwa wanachama,kuiwezesha CHAMUDATA kuwa karibu na serikali ili kutatua changamoto zinazowakabili,kuhakikisha bendi zote zinazofanywa maonyesho zimesajiliwa BASATA pamoja na kuandaa Tamasha kubwa la Muziki wa Dansi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Bw.Said Kibiriti amesema kwamba uongozi uliopo Kwa sasa ni uongozi mpya,baada ya kukabidhiwa ofisi na uongozi wa zamani baadhi ya nyaraka za ofisi hazipo nakwamba baada ya kufatilia wamebaini baadhi ya viongozi hao wameshafariki,hivyo kumekuwepo na madeni huku akaunti za chama za NMB na CRDB zikiwa hazina fedha.

" Hatuna Hesabu Sahihi ya madeni kwa sasa,lakini bado tunaendelea kuyakusanya na yakiwa tayari tutawafahamisha wanachama,kwasasa tuanaendelea kukiimarisha chama kwani kimeanzishwa tangu mwaka 1986 lakini bado kimekuwa hakifahiki vizuri kwa wanamuziki wa Dansi Nchi nzima" amesema Bw.Kibiriti.
Mwenyekiti wa chama cha Muziki wa dansi nchini (CHAMUDATA) Luizer Mbutu akizungumza na Waandishi wa habari juu ya muelekeo wa Chama hicho Kwa uongozi mpya ulioingia madarakani ukiongozwa na yeye mwenyewe akiwa kama Mwenyekiti wa chamudata
Katibu Mkuu wa chama cha Muziki wa dansi nchini (CHAMUDATA) Said Kibiriti akibainisha kuwa madeni yanayoikabili chama hicho yatashughulikiwa na uongozi huo mpya kutokana na uongozi wa awali wengi wao wameshafariki



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini