Na.Khadija Seif, Michuzi Tv.
KUKUA Kwa Sekta ya Mitindo na Ubunifu nchini umechagiza kupatikana kwa fursa mbalimbali za ajira kwenye majukwaa pamoja kazi za kibunifu Kwa nia ya kuthamini na kuwainua vijana wa kitanzania kiuchumi.
Akizungumza wakati wa usahili wa wanamitindo uliofanyika katika ukumbi wa rhapsody coco beach jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la "Tanzania fashion Festival" Deogratius Kithama amesema ni wakati wa wadau wa mitindo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 kuhakikisha vijana wanapata ajira katika Kila Sekta hivyo akiwa kama mmoja ya wadau wa Sekta ya mitindo ni miaka 5 ameendelea kushika Mkono vijana wenzake kuhakikisha wanapata nafasi ya kukuza vipaji vyao.
"Serikali imeweka nafasi Kwa vijana wengine kuwapa fursa vijana Ili tuwe na Taifa lenye ajira kwa wingi kupitia fursa mbalimbali zinazotolewa hivyo jukwaa la Tanzania fashion Festival limetoa fursa zisizozakudumu kwa vijana mbalimbali Kwa takribani miaka 5 kila mwaka kwani kupitia wanamitindo wanapata Fedha hata wabunifu pia wanapata nafasi hiyo."
Aidha,Kithama ameeleza kuwa muitiko wa Tamasha hilo limekuwa kubwa kadri siku zinavokwenda na kupelekea uhitaji wa Wana mitindo kuongezeka na kufikia 30 ikijumuisha kwa wanaume na wanawake pia pamoja na wabunifu kutoka sehemu mbalimbali idadi ikiwa zaidi ya 30 kutoka bara na visiwani akiwemo Jamila Vera swai, Bahati zanzibar,Waiz, Victoria Martin na wengine wengi.
Hata hivyo Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika agosti 27 mwaka huu katika ukumbi wa Slipway na litahudhuriwa na Mgeni wa heshima Miriam odemba ambae anathamini mchango wake katika tasnia ya Ubunifu na wanamitindo nje na ndani ya Taifa la Tanzania huku burudani ikitolewa na Msanii Damian soul.
"Jukwaa la mwaka huu kutakuwa na burudani mbalimbali ya muziki miongoni mwao ni Mwimbaji Damian soul Kwa Sababu mitindo inashabihiana na Muziki na Mgeni wetu wa kutufungulia jukwaa letu ni Miriam odemba ".
Wanamitindo waliofanikiwa kuchaguliwa kuonyesha uwezo wao katika jukwaa la "Tanzania fashion Festival " lililoandaliwa na mdau wa kazi za Ubunifu nchini Deogratius Kithama akiwa pamoja na wabunifu na majaji na warembo waliochaguliwa jijini Dar es salaam
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments