Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
MAOMBI ya Watazamaji wa kipindi cha Mr.Right yamesikilizwa, Msimu wa 3 watu maarufu wamealikwa kwenye kipengele kipya kuleta kinogesho cha kipindi hicho
LULU diva ambae ni mshauri wa kipindi hicho cha Mahusiano amewakaribisha watazamaji wa "Hello Mr Right na kuhaidi Msimu huu watazamaji watapata vionjo tofauti tofauti katika Msimu wa 3 wa reality show hiyo.
Akizungumza wakati wa kutambulisha Msimu wa 3 wa kipindi hicho kinachorushwa katika chaneli ya St bongo katika king'amuzi cha Startimes, Mkurugenzi wa Tv3 Ramadhani Msemo amesema kutokana na Maombi mbalimbali yaliyojitokeza kuwepo katika kipindi wameamua kufanya maboresho Ili kunogesha kipindi hicho Kwa kusikiliza zaidi watazamaji wanataka vitu gani.
"kutokana na Maombi mengi kuhusiana na maboresho ya kipindi hiki tumeamua kuongeza nafasi ya watu maarufu,wenye ushawishi kwenye jamii kuwepo kama sehemu ya kuwapa neno washiriki hao ikijumuisha wanamichezo,wasanii na watu wengine wenye nguvu katika nchi hii"
Aidha,Mshauri wa kipindi hicho chenye maudhui ya Mahusiano Lulu Abas maarufu kama "Lulu diva" amesema ataendelea kutoa ushirikiano baina yake na washiriki wote katika vizimba vyao ili kuwahakikishia wanapata wenzao wao Huku vigezo na masharti vikiwa vimezingatiwa.
Hata hivyo Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes David Malisa amesema mwaka huu wamekuja na vipindi vya bandika bandua Ili kuendelea kubeba Maudhui ya kinyumbani zaidi na kuwa fursa vijana wengi.
Malisa ameongeza kuwa kipindi hiko kitakua kikiruka kila siku ya jumamosi saa 4 usiku na marudio yake siku ya jumapili jioni.
Huku akiwasihi watazamaji kulipia vifurushi vyao kwa wakati Ili wasipitwe na uhondo wa msimu huo wa 3 kauli mbiu ikiwa "Kazi kwako''.
Meneja Masoko wa Kampuni ya startimes David Malisa akizungumza utofauti wa Msimu mpya wa kipindi cha hello Mr.Right Huku akitambulisha ingizo jipya la kipengele cha watu Mashughuri kualikwa katika kipindi hiko
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments