NMB YATANGAZA USHIRIKIANO NA KITUO CHA RADIO CHA EFM NA TVE KAMA WASHIRIKI WENZA MBIO ZA NMB MARATHON 2022. | ZamotoHabari



Benki ya NMB imetangaza ushirikiano na kituo cha Radio cha EFM na TVE kama washiriki wenza katika mbio za NMB Marathon 2022 zinazotarajiwa kufanyika Septemba 24, 2022 katika Viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku kauli mbiu ikiwa “Mwendo wa Upendo”.

Mbio hizo zenye lengo la kurudisha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya fistula kwa kukusanya Sh. milioni 600 ambazo zitaenda kuwasaidia na matibabu katika Hopsitali ya CCBRT.

Akizungumza jana katika uzinduzi huo uliofanyika katika jengo la studio za EFM na TVE, Kaimu Mkuu wa Habari na Mawasiliano kutoka NMB, Vicent Mnyanyika alisema kuwa katika marathon iliyofanyika mwaka jana ambayo ilifanya vizuri hakukuwa na mshirika wa chombo cha habari hivyo msimu huu tumeamua kushirikiana na kituo cha radio cha EFM na TVE katika kukamilisha malengo ya kukusanya Sh. milioni 600.

“Mbio zetu zitakuwa za aina tatu kilometa 5, kilometa 10 na kilometa 21 na gharama zake ni Tsh 20,000 kwa 5km, Tsh 20,000 kwa 10km na Tsh 30,000 kwa 21km.Tukio letu litakuwa kuanzia asubuhi mpaka jioni, baada ya kumaliza mbio, zawadi mbalimbali zitatolewa na kisha tuburudike na wasanii mbalimbali,” alisema

Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka EFM na TVE, Denis Busulwa (Ssebo) alisema furaha ya EFM na TVE kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuinua masuala ya kijamii huku akiamini ushirika wa EFM Na NMB ni ushirika mkubwa unaokutanisha chapa (brand) bora katika kunyanyua masuala ya afya.

Tutakuwa na pre party ya masaa 20 kuelekea siku ya Septemba 24, baada ya hapo washiriki wote waliojisajili watapata nafasi ya kupata supu katika eneo hilo hilo kwa pamoja kisha kuchukuliwa na basi litakalowapeleka mpaka katika viwanja vya Leaders.

Jisajili na NMB Marathon kupitia https://marathon.nmbbank.co.tz/ uwe sehemu ya kurudisha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya Fistula.

Kaimu Mkuu wa Habari na Mawasiliano, Bw. Vicent Mnyanyika (wa pili kushoto) kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka EFM na TVE, Bw. Denis Busulwa (Ssebo), Mratibu wa mbio NMB Marathon – Suleiman Nyambui na Meneja wa Mbio, Bw. David Marealle wakishikina mikono kuonesha ishara ya upendo kwenye kutangaza kituo cha radio cha EFM na TVE kama washiriki wenza.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini