TANZANIA FASHION FESTIVAL 2022 YAACHA GUMZO | ZamotoHabari


Na.Khadija Seif, Michuzi Tv

JUKWAA la Ubunifu nchini (Tanzania Fashion Festival) Msimu wa 5 lafana wabunifu wampa heko Kithama Kwa kutambua Mchango wake katika tasnia ya Ubunifu wa Mavazi nchini .

Akizungumza na Michuzi Muasisi wa jukwaa hilo Deogratius Kithama amesema kila Msimu kunakua na utofauti kwani msimu huu wamechukua warembo wengi kutokana na muitikio kuwa mkubwa zaidi na kupelekea kuwapa nafasi zaidi.

Hata hivyo amesema jukwaa hilo linafungua fursa mbalimbali ikiwemo Kwa wanamitindo wenyewe hadi wabunifu nje na ndani ya nchi kujulikana kutokana na wageni wanaohudhuria kupenda bunifu zinazopita jukwaani.

Aidha, ameeleza kuwa mwakani wanategemea kuandaa Msimu ambao utakua tofauti zaidi Ili kunogesha jukwaa hilo lenye kufungua fursa za kibiashara na kuwaomba wadhamini wajitokeze Kwa wingi.

Jukwaa hilo limefanyika katika ukumbi wa terrace jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Mgeni wa heshima ambae ni Mwanamitindo nchini Miriam odemba nakusema ni wakati wa Tasnia ya Ubunifu kukuwa kutokana na kuwepo Kwa wadau ambao wanatoa ushirikiano zaidi kwenye Sekta hiyo.

Wabunifu mbalimbali walipata nafasi ya kuonyesha kazi zao akiwemo Enjipai, Victoria Martin pamoja na watu maarufu akiwemo Madam Ritha Paulsen ,Noel ndala ,Wema Sepetu Huku burudani ikitolewa na Msanii wa Muziki wa hip-hop Damian Soul pamoja na mpigaji wa chombo cha kinanda cha mdomoni.

Mbunifu wa Mavazi nchini Enjipai akipita jukwaani na warembo wakiwa wamevalia bunifu zake katika jukwaa la Tanzania Fashion Festival lililofanyika katika ukumbi wa terrace jijini Dar es salaam.
Msanii wa miondoko ya hip hop Damian soul akitumbuiza katika jukwaa la Tanzania Fashion Festival lililoandaliwa na Deogratius Kithama likiwa ni Msimu wa 5 tangu kuanzishwa kwake.
Muasisi wa jukwaa la Tanzania Fashion Festival Deogratius Kithama akiwa na Mgeni wa heshima Miriam odemba akizungumza machache mara baada ya kuwasili katika jukwaa hilo 

 


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini