Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said amepelekwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) baada ya Sekretarieti ya Maadili ya Shirikisho hilo kumfungulia mashtaka ya kimaadili sanjari na Afisa Habari wa Klabu hiyo, Haji Manara.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, imeeleza kuwa Mhandisi Hersi amefunguliwa mashtaka hayo kwa kwenda kinyume na ibara ya 16 (1) (a) ya Katiba ya TFF, pamoja na Ibara ya 1(16) ya Katiba ya Yanga.
“Kamati ya Maadili ya TFF hivi karibuni ilimfungia miaka miwili Manara kujihusisha na shughuli yoyote ya mpira wa miguu (any football-related activity), lakini ameshindwa kutekeleza adhabu hiyo”.
“Baada ya Manara kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya TFF, Sekretarieti ilimwandikia barua Mhandisi Said kuhakikisha Klabu yake inaheshimu uamuzi huo”, imeeleza taarifa
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF tayari amepelekewa mashtaka hayo, walalamikiwa watapewa mashtaka na mwito mara baada ya Kamati hiyo kupanga tarehe ya kusikiliza mashtaka hayo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments